Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Mwisho
wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya
kuanzisha na kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa
mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano
Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo
la ukosefu wa ajira.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.

Baadaye
mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama
Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch
Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar
waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni