Meneja wa mawasiliano wa Jovago,Liliani Kisasa akizungumza na
waandishi wa habari juu ya kutumia mitandao ya kijamii kwa maendleo ya
Taifa katika mkutano uliofanyika kinondoni jijini Dar es Salaam.
TAASISI
ya kufanya Biashara mitandaoni ya Jovago Tanzania imewataka watanzania
kutumia fursa ya matumizi ya mitandao ya kijamii kuitangaza nchi katika
sekta ya utalii kimataifa.
Wito huo imetolewa na Mkurugenzi wa Jovago Afrika Mashariki
Estelle Verdier –Watine alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao wa Instagram
kutangaza utalii wa Tanzania.
“Tanzania ni nchi inayoongoza kwa matumizi ya instagram Africa
hivyo fursa hiyo ni vyema ikatumika vyema katika kupandisha utalii wa
taifa hili kuliko kupost vitu ambavyo avina faida kwa taifa” alisema
Estelle.
Alisema kuwa kwa kuthamini hilo tasisi ya Jovago Tanzania imeandaa
shindano la kuweka pichakatika Insrgram hivyo atakaye pata like nyingi
ataweza kupata ofa ya kulala katika Hotel ya Ramada iliyopo Mbezi Beacha
Dar es Salaam.
Kwa upande wake afisa habari wa kampuni hiyo Liliani Kisasa
aliwatka watanzania kuchangamkia fursa hiyo hili waweze kufurahia siku
hiyo wakiw ana wenzi wao.
Alisema ni jambo zuri sana kama mmoja ya watu kutoka hapa nchini.
Liliani Kisasa PR manager Jovago.
Liliani Kisasa PR manager Jovago.
Estelle Verdier -Watine East Africa Manger Jovago .Com akizungumza na wana habari.
Liliani Kisasa PR manager Jovago akiojiwa na ITV.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni