Alaigwanani
wa mila, Saibulu Olemariki akimuongoza Mkurugenzi wa Idara ya uratibu
maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kukagua athari
za upepo kwa mashamba ya migomba kijiji cha Mungere, wilayani
Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani
wa mila, Saibulu Olemariki akionesha sehemu ya mgomba iliyoanguka
baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya
uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa
hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari ,
2016.
akimueleza
jambo Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki mara baada ya kukagua
athari za upepo kwa mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere,
wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani
wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu
maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya baadhi ya
ndizi zilizo katwa kwenye migomba iliyoanguka baada ya upepo mkali
kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika
kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani
wa mila, Saibulu Olemariki akimshika bega Mkurugenzi wa Idara ya
uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kama
ishara ya kumshukuru mara baada ya kukagua athari za maafa ya upepo
mkali katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari ,
2016.
Alaigwanani
wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu
maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya maeneo upepo
mkali ulioleta maafa katika mashamba ya migomba katika kijiji cha
Mungere, wilayani Monduli, mara baada ya kukagua athari za maafa hayo
, tarehe 31 Januari , 2016. (Picha na Ofisi ya Wazairi Mkuu )
Na. Mwandishi maalum
Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa itatoa mbegu bure
za miti ili kukabili maafa ya upepo mkali kwa wakazi 3,000 wa kijiji cha
Mungere, ambao mashamba yao ya migomba yalikumbwa na maafa ya upepo
mkali uliosababisha ekari 250 kati ya ekari 300 za mashamba hayo
kuathiriwa na upepo huo.
Akiongea
wakati wa ziara ya kukagua athari za maafa hayo katika kijiji cha
Mungere, wilayani Monduli Tarehe 31 Januari, 2016, Mkurugenzi wa Idara
ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya
amebainisha kuwa serikali imeamua kuwagawia bure mbegu za miti
itakayopandwa kwa kuzunguka mashamba yao ili waweze kukabili maafa hayo
ya asili.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu idara ya uratibu maafa inalojukumu la kuratibu shughuli
za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya
kawaida pindi maafa yanapotokea kwa hapa kijijini Mungere tumeamua
kukabili maafa yatokanayo na upepo kwa kuwapa wakulima wa zao la ndizi
waweze kuipanda miti hiyo itakayowezesha kupunguza kasi ya upepo mkali
ambao husababisha migomba kuanguka katika mashamba yao.” amesema Brig.
Jen. Msuya
Msuya
aliongeza kuwa idara yake itatoa chakula cha msaada kwa waathirika wa
maafa hayo ili waweze kuwa na chakula cha kutumia wakati baadhi ya
migomba yao iliyoathirika ikiendelea kuchipuka na mingine kukomaa
ambapo wataweza kupata chakula lakini pia na kujipatia fedha kwa kuuza
zao hilo.
Awali
akiongea katika ziara hiyo, Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki
alifafanua kuwa upandaji miti ndio njia pekee ya kuwajengea uwezo
wakulima wa zao la ndizi kuweza kukabili maafa ya upepo katika kijiji
hicho kwa kuwa mashamba yao yamekuwa yakikumbwa na maafa ya upepo mkali
ambao umekuwa ukiangusha migomba ambayo tayari inakuwa imeshabeba ndizi
kubwa na zilizo komaa.
“Kama
kiongozi wa kimila nitawahamasisha wanakijiji wenzangu hasa wakulima wa
mashamba ya migomba kuhakikisha kuwa kila mtu anazungusha miti ya
kutosha katika shamba lake lakini pia kuhakikisha kuwa miti hiyo
inatunzwa kwa kuimwagilia maji na kutokatwa ovyo.” alisisitiza
Alaigwanani Olemariki.
Alaigwanani
Olemariki alieleza masuala yanayo kuwa kikwazo kwa wakulima hao kuwa ni
miundo mbinu ya barabara na Umwagiliaji kwa kueleza kuwa pamoja na
kijiji hicho kuwa na maafa ya upepo ambayo huathiri mashamba yao ya
migomba lakini pia miundo mbinu ya barabara imekuwa kikwazo cha wakulima
hao kwa kushindwa kusafirisha ndizi ili waweze kulifikia soko kwa
wakati .
“Tunaomba
serikali iweze kuiboresha barabara inayokuja kijijini hapa ili kuweza
kuhamasisha wafanyabiashara wengi kufika kijijini hapa kununua ndizi kwa
kuwa kama tunakuwa hatujapatwa na maafa tunaouwezo wa kuzalisha ndizi
nying na hili niombe serikali kuwa sisi tunazalisha ndizi nyingi amabazo
tukijengewa mazingira mazuri ya kilimo chetu ikiwa ni pamoja na
kujengewa mfereji bora wa maji tunao uwezo wa kuilisha Monduli nzima na
hata nje ya hapo.” alisisitiza Alaigwanani Olemariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni