Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la
kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji
miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba
alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya
maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa
Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji
miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama
Januari 27.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV
Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya
shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe
aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro
mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
Wasamaria
wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha
MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro,
wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani),
wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji
zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi
ya vitu vikiokolewa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya,
akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya
kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni