WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROF,JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA YA TANAPA.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof,Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Dkt Chanasa Mpelumbe Ngeleja.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof Wineaster Anderson

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof,Alexander Songorwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi Devota Mdachi mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanika katika ukumbi wa Mhakama ya Afrika jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini iliyomaliza muda wake Modestus Lilungulu walpkutana katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya .
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo akifanya utamburisho wa wajumbe wa bodi ya Wadhamini wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Wineaster Anderson ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii endelevu Afrika (NARESTi Africa) akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Dkt Lucy Lugwisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Alexander Songorwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Kamishna Marijani Nsato ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya jeshi la Polisi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Dkt Chanasa Mpalumbe Ngeleja ambaye pia ni Daktari Mkuu wa Mifugo ,Wizara ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,George Fumbuka ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Core Securities akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Devota Mdachi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyomaliza muda wake ,Modestus Lilungulu akitoa salam zake wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya TANAPA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo.katikati ni Mkurugenzi wa TANAPA,Allan Kijazi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) muda mfupi baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo.

UJENZI WA BARABARA ZA JUU ( FLYOVERS ) WAFIKIA ASILIMIA 19

Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui, Bw.Kiyokazu Tsuji (wa kwanza kulia) akionesha hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman.
Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman (mwenye shati ya mikono mifupi) akitoa ushauri kwa wahandari wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa bararabara za juu jijini Dar es Salaam.
Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Omari Athuman (kulia) akiongea na Ofisa Mshauri wa masuala ya usalama kazini, Bw. Richard Barwan wakati wa ziara ya Timu ya Mipango katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.


Na Adili Mhina, Dar.

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imefanya ziara katika Mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) unaoendelea katika makutano ya barabara za Nyerere/Mandela Jijini Dar es salaam na kuelezwa kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 19.2.
 

Ziara hiyo iliyofanyika hivi karibuni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi huo ilitoa fursa kwa Bw. Kiyokazu Tsuji, Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo inayotekeleza ujenzi huo kueleza maendeleo ya ujenzi kwa wataalam kutoka Tume ya Mipango.

Mhandisi huyo alieleza kuwa malengo ya awali yalielekeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba 2016, utekelezaji uwe umefikia asilimia 21.2 lakini lengo hilo halikufikiwa kutokana na moja ya mashine kupata hitilafu na kulazimika kuagiza wataalam kutoka nje ya nchi kuja kuifanyia matengenezo.

Hata hivyo Mkandarasi huyo alieleza kuwa tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafidia muda uliopotea wakati mashine hiyo ilipokuwa haifanyi kazi ili ujenzi wa barabara hizo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

Nao walaalam kutoka Tume ya Mipango walieleza kuwa Serikali na Wananchi kwa ujumla wanatarajia kuwa ujenzi huo utakamilika kwa muda uliopangwa hivyo Mkandarasi huyo ana wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

Wataalamu hao pia walimshauri Mkandarasi huyo kuwa ni vyema akawapeleka nje wataalam wanaoziendesha mashine hizo ili waweze kupata ujuzi na uwezo wa kutengeneza mitambo pale inapohitajika badala ya kusubiri watu kutoka nje kuja kufanya kazi hiyo. 

Walieleza kuwa kuwepo kwa wataalam wa ndani wenye uwezo wa kutatua hitilafu zinazojitokeza katika mitambo itasaidia kupunguza gharama na kuokoa muda ili kufanya mradi uende bila kusimama.
 
Ujenzi huo unaotekelezwa kwa miezi 35 kauanzia Disemba 1, 2015 hadi Oktoba 31, 2018 unalenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.

MWISHO

JOE BIDEN AMTAKA RAIS MTEULE DONALD TRUMP KUACHA 'UTOTO'

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden amesema rais mteule Donald Trump anapaswa kukua, na amemkosoa kuhusiana na hatua yake ya kushambulia vyombo vya Kiitelijensia.

Kauli hiyo ya Bw. Biden, ameitoa huku Bw. Trump akitarajiwa leo kupata maelezo kutoka kwa vyombo vya kijasusi vya Marekani kuhusiana na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani.

Bw. Biden amesema kwamba ni kutokuwa na akili kwa rais mteule kutokuwa na imani na vyombo vya Kiitelejinsia.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MGODI WA MAKA YA MAWEWA NGAKA UNAO MILIKIWA NA TANCOUL ULIOPO NAGAKA WILAYA YA MBINGA MKOA WA RUVUMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tancoul Bwana Mark McAnderew wakati alipotembelea mgodi wa makayamawewa Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo la taifa (NDC) Mlingi Mkucha wakati alipotembelea mgodi wa makayamawe wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe. Picha na Chris Mfinanga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mkawamawe ulivyo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Ruvama Mhandisi Mahenge pamoja naviongozi mbalimbali walipokuwa wanatemmbelea mgodi wa Ngaka. Picha na Chris Mfinanga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Rasilimsilimali watu wa kampuni ya Tancoul Ms Pendo Mweli wakati alipotembelea mgodi wa makayamawe unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo Ngaka wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shughuli za uchimbaji wa makayamawe unavyo fanywa nakampuni ya Tancoul katika mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la maendeleo la taifa NDC Dr Samuel Nyantahe

DONALD TRUMP AKWEPA KUISHUTUMU URUSI KWA UDUKUZI UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

Ripoti ya Kiintelejensia ya Marekani imesema rais wa Urusi Vladimir Putin aliamua kumsaidia Donald Trump kushinda uchaguzi wa urais wa Marekani.

Ripoti hiyo imesema kuwa kiongozi huyo wa Urusi aliagiza kufanyika kampeni yenye lengo la kujenga ushawishi wa matokeo ya uchaguzi.
Baada ya kupewa taarifa hiyo rais mteule Bw. Trump alisita kuishutumu Urusi kwa kitendo hicho na badala yake alisema kuwa hata hivyo matokeo ya uchaguzi hayakuathiriwa.
               Rais wa Urusi Vladmir Putin anashutumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani

RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA MAENEO YALIOATHIRIKA NA TETEMEKO NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO MKOANI KAGERA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa shule ya Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU