Umati wawatu uliouthuria katika zoezi la kuaga marehemu hao
Na Woinde Shizza,Arusha
MAKAMU
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa taTanzania Samia Suluhu ameongoza
maelfu ya waombolezaji katika zoezi la kuaga miili ya wanafuzi 35 wa
shule ya Luck Vicent ikiwemo walimu wawili pamoja na dereva mmoja
waliofariki katika ajali iliyotokea juzi eneo la Rotia wilayani karatu
mkoani Arusha.
Akizungumza
katika tukio hilo ambalo ni kubwa kutokea mkoani arusha na tanzania kwa
ujumla alisema kuwa kama serikali walmelipokea kwa masikitiko makubwa
na kwamba watajitahidi kuungana na familia zilizopoteza watoto wao ambao
hata wazazi wao walikuwa na malengo mazuri juu ya kuwapatia elimu bora
,huku akiwaagiza madereva wote kuzingatia sheria za barabarani na
kuepuka vilevi.
Alisema
kuwa ajali nyingi zinatokana na uzembe wa madereva na hivyo kuwataka
madereva wote kuwa makini pindi wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto
ili kuepuka ajali ambazo zinqweza kuzuilika.
"Serikali
yetu kwa sasa inapiga vita sana madereva walevi pindi wanapokuwa
wanaendesha vyombo vyao hivyo naomba tu kuagiza madereva wetu kuwa
makini na waadilifu kwani hata ajali kama hizi ambazo zinapoteza nguvu
kazi zinatokana na vilevi vinavyotumiwa na madereva na hivyo kuleta
maafa kama haya"aliongeza Samia.
Aidha
aliwataka pia madereva kuhakikisha wanabeba idadi ya watu wanaolingana
na uhalisia wa gari kwani wengi wao wamekuwa wakibeba idadi kubwa na
hivyo kusababisha madhara mkubwa zaido pindi ajali zinazotokea mfano wa
ajali hii.
Samia
alitumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya elimu ,jeshi la polisi kuwa
makini kuhakikisha sheria za barabarani zinazingatiwa ili kuepuka vifo
vya watoto.
Awali
mara baada ya kuwasili kwa miili hiyo 35 majira ya saa tano na robo
uwanjani hapo Vilio ,majonzi na simanzi vilitawala katika uwanja huo
huku watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa shule wakiwa wanazimia na
kuwahishwa mahospitalini ili kupatiwa huduma ya kwanza.
Aidha
katika zoezi hilo la kuaga miili ya wanafunzi hao serikali ya mmkoa wa
arusha ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo imeweza kugaharamia
shuguli zote za mazishi ya wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kutoa magari
ya kusafirisha miili hiyo mpaka eneo ambalo familia imejiwekea
utaratibu wa kuhifadhi miili hiyo ambapo miili 25 itasafirishwa nje ya
mkoa wa arusha,huku miili 10 ikibaki kwa taratibu za mazishi ndani ya
mkoa huu.
Hata
hivyo akiongoza misa ya kuaga miili hiyo kwa upande wa wakristo Askofu
wa kanisa la katoliki jimbo la arusha Josphat Lobulu alisema kuwa siku
za mwanadamu ni chache hivyo inawapasa wanadamu kuishi maisha ambayo
yanaendana na mapenzi ya Mungu.
Alisema
kuwa vifo vya wanafunzi hao kimesikitisha kila mtu kwa kuwa wamekufa
wakiwa malaika wa Mungu wakiwa bado wanahitajika na taifa la sasa.
Hata
hivyo zoezi hilo la kuagwa kwa miili hiyo limeudhuriwa na viongozi
mbali mbali kutoka serikalini na nje ya nchi wakiwemo waziri wa elimu wa
tanzania ,waziri wa elimu kutoka nchini kenya,jaji mkuu wa mahakama
,jaji mstaafu ,waziri mstaafu lowasa na Sumaye ,viongozi wa kambi ya
upinzani bungeni,madaktari kutoka nje ya nchi pamoja na wabunge mbali
mbali.
Aidha
tukio hili lilitokea mei 6 wilayani karatu ambapo wanafunzi hawa
walikuwa wanenda kufanya mitihaninya ujirani mwema katika shule ya
Tumaini na ndipo costa ilifeli breki na kusababisha vifo 35 na majeruhi
watatu ambao ni Doreen Mshana (13),Sadia Ismaili (11) pamoja na Wilson
Tarimo (11)wote wakazi wa Morombo ambapo wote wamelazwa katika hospitali
ya mkoa ya Mount meru wakiendelea na matibabu.
Wananchi wakiwa nje ya uwanja mara baada yakushindwa kuingia ndani kutokana na wingi wa watu
Miili ya marehemu ikiwasili katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid tayari kwa zoezi la kuagwa
Mmoja wa mwanafunzi akiwa amebebwa na wahudumu wa chama cha msalaba
mwekundu mara baada ya kuzidiwa na kuanguka ndani ya uwanja wa Sheikh
Amri Abeid wakati alipokuja kuaga wanafunzi wenzake (picha zote na
Woinde Shizza,Arusha)
Umati wa watu ukiwa unalia kwa uchungu
Mbunge wa viti maalumu Amina Mollel akiwa analia kwa uchungu mara baada ya kuaga miiili ya marehemu hao
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg:Jokate Mwengeloakiwa
anatoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliobeba miiili ya wanafunzi
hao
Zoezi la kuaga mwili likiendelea huyu ni mmiliki blog ya fatherkidevu nae akitoa heshima za mwisho
Picha za majeneza ya wanafunzi hao 32 pamoja na walimu na dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo
Mmoja wa Mama aliofiwa na mtoto wake akiwa analia kwa uchungu mara
baada ya miili ya watoto hao kuanza kuwasili katika kiwanja cha
kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid