WAZIRI MKUU, MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA SADC GABORONE


Z8
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama  uliopo  Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Z9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

POLISI WAPAMBANA NA WANANCHI VURUGU ZA KUFUNGA BARABARA MKWAJUNI KINONDONI


MKW1
Katika maeneo ya Mkwajuni Kinondoni baadhi ya wananchi wamefunga barabara wanachoma matairi kwa kile wanachodai kupinga bomoa bomoa Askari wako eneo la tukio wakijaribu kuwazuia kufanya matukio hayo na hakuna magari yanayoweza kupita eneo hilo kutokana na vurugu zilizoababisha  kufungwa kwa barabara hiyo ya kutoka Moroco kwenda Magomeni.
MKW2 MKW3

JIJI LA ARUSHA LAJIPANGA KUONDOA MAKAZI HOLELA

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akiweka saini makubaliano kati ya Jiji la Arusha na kampuni ya Bondeni Seeds Limited yatakayowezesha eneo la Heka 750 kupimwa na kuwa kwenye mpango unaoendana mpango Mji wa Jiji katika eneo la Murieti wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita,Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema,Mwanasheria wa Jiji,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd na Mwanasheria wa Bondeni Seeds Limited leo
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akibadilishana hati za makubaliano  na Mkurugenzi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited ,Rakesh Vohora  ya kuendeleza eneo la Heka 750 eneo la Muriet linalomilikiwa na kampuni hiyo .
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza  baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo,kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro.

Diwani wa Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji la Arusha,Metson Paul(kushoto) akiwa Mwanasheria  na Mkurungezi wa  kampuni ya Bondeni Seeds Limited.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo.

Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya  Jiji .

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.

"Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.

Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.

Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.

KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHILISHWA.


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.

Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae kuahilishwa kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea kusikilizwa kuanzia majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na moja jioni.
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani) akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema)

WAZIRI WA MAMBO YA NJE USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKUTANA NA WABUNGE AFRIKA MASHARIKI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” AlisemaMh. Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.

Bunge la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
 Dkt. Mahiga, akisaliamiana na mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji
 Mh. Shy-Rose Bhanji akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (wakwanza kushoto) na maafisa wengine wa wizara hiyo, mara baada ya kikao hicho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Makongoro Nyerere, akipena mikono na Bi. Mindi Kasiga

WACHUUZI WA TANZANITE WALIA NA LESENI


 
Na Mahmoud Ahmad
WACHUUZI wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba Serikali kutowabana walipe leseni ya ununuzi, kwani uwezo wao ni mdogo na wao ni madalali siyo wanunuzi wa madini hayo.
Wakizungumza juzi wachuuzi hao walidai kuwa hawapingi kulipa mapato ya serikali ila zoezi la ulipaji wa leseni ya kununulia madini ya Tanzanite ingetakiwa kutekelezwa kwa wafanyabiashara peke yao na siyo kwa wachuuzi wadogo.
Mmoja kati ya wachuuzi hao Anturusia Chande alisema wengi wao wanapewa madini hayo na kuzunguka kwenye masoko ya Mirerani kwa lengo la kujikimu maisha yao ikiwemo kusomesha watoto, mavazi, chakula na matibabu.
“Sisi hatuvuki na madini nje ya eneo la Mirerani na tunategemea kuendesha maisha yetu kupitia uchuuzi huu mdogo mdogo na pia hatuna mtaji kwani tumejiajiri wenyewe serikali ituangalie kwa kupitia hili,” alisema Chande.
Alisema wao wanachangia pato la Taifa kupitia sekta hiyo kwa kulipa kodi pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali madukani ikiwemo sukari, mchele, mafuta ya kula, ya taa, sigara na nyinginezo ila bado wanasumbuliwa na serikali.
Kaanael Minja alisema zoezi la kuwakamata wachuuzi ambao hawakulipa leseni lililoendeshwa wiki iliyopita, halikufanyika kwa haki kwani kuna baadhi yao waliporwa madini ambayo siyo yao na hawakurudishiwa hadi hivi sasa.
“Kabla ya kuendesha kamata kamata hiyo wangetoa elimu kwanza kwa wachuuzi hao lakini kitendo cha kufika kijiweni na kuanza kuwakamata watu wasio na leseni siyo kizuri, wangepaswa kuwaelimisha kwanza,” alisema Minja.
Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahmoud Kambona aliwataka wachuuzi hao kujipanga na kulipia leseni ya ununuzi wa madini hayo ili waongeze mapato kwa serikali ambayo inawaletea wananchi maendeleo.
“Wanatakiwa kutambua kuwa hiyo ni sheria ambayo imepitishwa na sasa kinachotakiwa ni utekelezaji kwani serikali zote hujiendesha kutokana na kodi ambazo zinalipwa na wananchi wake na siyo vinginevyo,” alisema Kambona.

DC ATOA WIKI MBILI WANAFUNZI WAENDE SHULE



Na Mahmoud Ahmad
Mkuu wa Wilaya ya SimanjiroMkoani Manyara, Mahmoud Kambona ameagiza
wanafunzi wote waliofaulu kujiunga nashule za sekondari wilayani humo
wawe wamewasili kwenye shule zao na kuanzamasomo baada ya wiki
mbili.Kambona alitoa agizo hilo juzialipokuwa anakagua shule ya
sekondari Msitu wa Tembo na kuzungumza na watendajiwa vijiji, kata,
madiwani na maofisa Tarafa, kuhusiana na wanafunzi waliofaulukujiunga
na masomo ya sekondari. Alisema wanafunzi wote waliofaulukujiunga na
sekondari wanatakiwa wafike kwenye shule zao baada ya muda wa
wikimbili kwa ajili ya masomo na endapo wasipotekeleza hilo
atawachukulia hatuakali viongozi wa eneo husika. “Nitawachukulia hatua
kali viongoziwote wakiwemo madiwani, maofisa tarafa, watendaji wa
kata, vijiji na wenyevitiwa vijiji wa sehemu husika ambao wanafunzi
wote waliofaulu watakuwa hawajafikashuleni,” alisema Kambona.Pia,
aliwaagiza wakuu wa shule zasekondari za wilaya hiyo kuwaelekeza
wazazi na walezi wa watoto ambao wamefaulukujiunga na shule zao, juu
ya majukumu yao na majukumu ya serikali kuhusiana naelimu bure.Baadhi
ya wazazi wa wanafunziwaliofaulu Joseph Odoyo na Mustafa Seif walisema
dhana ya elimu bure ya RaisJohn Magufuli bado hawajaielewa kwani
iliondolewa ni ada pekee ila chakula na mahitajimengine
wanachangia.“Ada ya sh20,000 ndiyo pekee iliyofutwaila tunachangia
huduma nyingine za mpishi sh15,000 kuni sh15,000 kusaga na
kukoboash15,000 kulima shamba la shule sh15,000 na viungo sh10,000 kwa
muhula mmoja,”alisema Odoyo.  Alisema pia wazazi wanatakiwa
kuchangiakilo 80 za mahindi, kilo 35 za maharage, kilo tano za sukari,
kilo 12 za mchelena lita tano za mafuta ya kula kwa muhula mmoja ila
sh5,000 ya muhuri wa nemboya shule imetolewa.