WANAUME WASINDIKIZENI WAKE ZENU KILINIKI

Festus Makwame wa Kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo la Arusha akiwa anafurahiajambo wakati akiwa anaendesha ibadaya mkesha wa sikukuu ya christimas hapo jana usiku Jijini Arusha.Picha naVero Ignatus Blog.
Baadhi ya waumini waliohudhuria katika ibada hiyo ya mkesha wa sikukuu ya Christmass ni pamoja na maharusi hawa .Picha na mahmoud ahmad
             Father Festus Makwame akiwa amembeba mafano wa mtoto Yesu aliyezaliwa ilipotimia majira ya saa sita kamili za usiku katika kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo la Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
fFather Festus Makwame akiwa anahubiri katika mkesha wa sikukuu ya christimasiliyofanyika katika kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo laArusha.






Maharusi Denis na bi Joviety wakiwa ibadani muda mfupi kabla ya kufunggishwa ndoa kanisani hapo.Picha na Vero Igantus Blog

Maharusi hawa bwana Charles na bi Sabilina waliweza kufunga ndoa katika mkesha huo wa sikukuu ya christma katika kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo la Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.


                              Na,Mahmoud Ahmad.Arusha.

Wito umetolewa kwa wanaume kuwa makini na kuwasindikiza wake zao kiliniki wakati wakiwa wajawazito kwani yapo mambo muhimu watakayojifunza wakiwa pamoja yatakayomsaidia mama na mtoto kuwa salama hadi wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa na father Festus Makwame wa kanisa katoliki Sent Treza jimbo la Arusha alipokuwa kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya krismas na kusema kuwa wanaume wengi hawana tabia ya kuwa na wake zao pindi wanapokuwa wajawazito jambo ambalo ni kosa kubwa

“Wanaume wasindikizeni wake zenu kiliniki huoni kwamba anashirikiana na Mungu katika uumbaji tena anakujengea heshima yawewe kuitwa baba Fulani?nenda nae yapo mambo mengi mtakayoelekezwa hata namna ya vyakula anavyotakiwa kula akisahau kwa vile ulikuwepo utamkumbusha?hebu igeni mfano wa Joseph na Maria hadi Yesu Kristo anazaliwa walikuwa pamoja.”alisisitiza

Amewataka waumini waliohudhuria ibada hiyo ya mkesha wa christmas waamue kubadilika waruhusu Kristo azaliwe mioyoni mwao ili mambo yao yawe mapya ,huku akisisitiza msamaha wa kweli pale mmoja anapomkosea mwingine kwani ni jambo ambalo Mungu analifurahia

“Wacha tuwe wakweli hakuna jambo gumu kama kumsamehe mtu aliyekukosea tena kwa makusudi,lakini kwa vile Mungu ameagiza tusameheane ni lazima tufanye hivyo na ukweli utabakia kuwa hivi Msamaha wa kweli ni ule ambao unautoa huku Unauma umekosewa lakini unasamehe kwa faida yako mwenyewe pia.”Alisisitiza father Festus.

Aidha amesema kuwa katika ibada hiyo ya mkesha wa krismas amewataka waumini kuachana mila na desturi potofu ambazo hazimpendezi Mungu kwani ni uvuli wa mauti.

“Wacheni michanganyo michanganyo kwani haimpendezi Mungu jamani kama umeamua kuwa kwa Mungu ,basi mfuate ili upate uzima wa milele ,na kama mwenzetu umeamua kumfuata shetani basi mfuate uangamie kwaani mambo haya ya michanganyiko michanganyiko mkiiendekeza huwa inaleta balaa na mikosi katika familia zenu”alisema father Festus.

BEN POL AWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA,NDANI YA MJENGONI CLUB JIJINI ARUSHA CHRISTMAS

Displaying
20161226_004941.jpg
Mwanamuziki wa kizazi kipya akiwasalimia wakazi wa Arusha mara baada ya kuingia katika ukumbi wa mjengoni Club awalikuwa wanamsubiria kwa shauku kubwa.Picha na mahmoud ahmad
Displaying
20161226_004732.jpg
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ben Pol akiwa anawapa burudani wakazi wa Jijini Arusha katika usiku wa kushehrerkea sikukuu ya Chrismass kwa katika ukumbi wa mjengoni Club.Picha na mahmoud ahmad
Displaying
20161226_020244.jpg
Waru wakila bata batandi katika usiku wa kusheherehekea sikukuu ya Christmas katika ukumbi wa mjengoni Club,na Mjengoni Classic Band pamoja na Ben Pol ilikuwa sheeda.Picha na mahmoud ahmad
Displaying 20161226_020229.jpg
Watu mbalimbali walifurahia Sikukuu ya Chrisrimas ndani ya Mjengoni Club,na Mjengoni Clsssic Band iliyopo Olasiti Jijini Arusha.Picha na mahmoud ahmad
Displaying 20161226_020229.jpg

Na.Mahmoud Ahmad Arusha

Mwanamuziki wa kizazi kipya Ben Pol ambapo kwa watu wengi wanamtambua kwa wimbo wake wa moyo mashine amezikonga nyoyo za wakazi wa Arusha walipokuwa wakisheherekea sikukuu ya Christimas katika ukumbi wa Mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha.

Awali kuliibuka uvumi kuwa msaniii huyo hatatokea katika shoo hiyo katika usiku huo wa kusheherekea sikukuu christimas jambo ambalo lilizua sintofahamu kwa baadhi ya watu walioingia ukumbini hapo kwaajili ya kumuona Ben Pol.

Blog hii ilipata muda wa kuzungumza na mkurugenzi wa Mjengoni Klub John Mdeme pamoja na Kiongozi wa Bendi ya Mjengoni Classic Robert Mukongya ili kutaka kufahamu kuhusiana na uvumi huo ndipo walipojibu kwa kusema kuwa hayo ni maneno tu ya upotoshaji .

"Jamani sijui nani kazileta taarifa hizi kwani Ben tulikuwa nae mchana kwenye shoo ya watoto ,sasa haya yametoka wapi binadamu bwana!mimi nakuaminisha Ben yupo na watu wote waliopo hapa watafurahi na kuburudika mioyoni mwao wala wasitie shaka"alisisitiza John.

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa waliamua kuwaandalia kitu kizuri wakazi wa Arusha kwa bendi ya Mjengoni Classic pamoja na Ben Pol kuwepo kuwapa raha wakazi wa Arusha na wageni mbalimbali kutoka nje ya Arusha na nchi mbalimbali waliokuja kusheherekea sikukuu wapate ladha tofauti na nzuri. 
 



 

SUALA LA KUACHIANA VITI VYA KUGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI KWA UMEOJA WA KATIBA YA WANANCHI BADO KIZUNGUMKUTI ARUSHA

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia akiwa na Viongozi wa CUF mkoa wa Arusha Mwenye shati la blue ni Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF)mkoa wa Arusha Zuberi Mwinyi baada ya mazungumzo ya ushirikiano wa ukawa Hotel ya Safari jijini Arusha picha na Maktaba

                                       
                                   
                                        Na Mahmoud Ahmad Arusha
Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge  kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru  ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.
Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.
Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.
Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.
“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.
Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.
Suala la mgawanyo wa maeneo ya kugombea limekuwa likivichanganya vyama hivi licha ya kuwepo makubaliano yaliofanywa na vingozi wa vyama vine hali inayoonekana kutokuwa na muafaka katika jambo hili, mfano majimbo ya segerea chadema na cuf walisimamisha wagombea na kujikuta wakiangukia pua katika jimbo hilo,hali inayoonyesha hakuna makubaliano katika hilo.
“tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi
Juhudi za wanahabari kuwatafuta viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa chama na Katibu wa Kanda ya kaskazini wa chama hicho Amani Golugwa ziligonga mwamba baada ya simu zao kutokupokelewa kila walipopigiwa bado juhudi zinaendelea kuwatafuta ili waweze kujibu madai hayo.
Mwisho…………………………..

MRADI WA GREEN VOICES WAFANIKISHA UTENGENEZAJI WA JIKO LA UMEME-JUA MOSHI

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, akisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi. Kushoto kwa Noela ni mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices Moshi, Farida Makame. Wengine pichani ni washiriki wa kikundi hicho. Uzinduzi wa jiko hilo lililotengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa Green Voices ulifanyika hivi karibuni mjini Moshi.
Jiko la umeme-jua ambalo limetengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa mradi wa Green Voices Tanzania kwa ajili ya kikundi cha akinamama wa TAWOCA Moshi. Jiko hilo linafaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uharibifu wa mazingira.
Wanakikundi wa TAWOCA Green Voices Moshi wakihakikisha jinsi joto la jua linavyosaidia kupika kwa kutumia jiko la umeme-jua. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko hilo, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, Robert George, pamoja na akinamama wakisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi.
Mhandisi Noela Byabachwezi, mwenye kofia kulia, akionyesha kwa vitendo jinsi jiko la umeme-jua linavyofanya kazi.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, Robert George – kulia – akisikiliza maelezo mbalimbali ya akinamama wa TAWOCA Green Voices Moshi kabla ya kuzindua jiko la umeme-jua.
                                                                                                                  Picha ya pamoja.

VIUNGA vya ukumbi wa Aroma mjini Moshi vimesheheni akinamama wengi katika siku hii ya Jumamosi, kama ilivyo kawaida kwa siku kama hiyo, ambapo wote wanaonekana kuwa na nyuso za furaha kutokana na mijadala inayoendelea.

Lakini tofauti na Jumamosi nyingine ambapo akinamama wa kikundi cha Wamama wa Kahawa ambao ni wanachama wa Tanzania Women Coffee Association - TAWOCA mjini humo kujadili masuala mbalimbali ya ujasiriamali, siku hii inaonekana kuwa ya tofauti kwa sababu licha ya idadi ya akinamama kuongezeka, lakini kuna tukio kubwa na muhimu ambalo limewakutanisha.

"Leo tunazindua rasmi jiko la umeme-jua, yaani parabolic solar cooker, ambalo kupitia udhamini wa mradi wa akinamama wa Green Voices, hatimaye limeweza kupatikana baada ya jithada za miezi kadhaa," ndivyo anavyoanza kuelezea Farida Makame, mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices wa kikundi hicho, huku akionyesha kifaa kinachofanana na dish kama la satellite ambacho katikati yake kumewekwa sufuria inayong’aa kama taa kubwa ya umeme.

Anasema kwamba, jiko hilo linaweza kupika kila aina ya chakula kwa kutumia mionzi ya jua ya moja kwa moja bila kuathiri mazingira.

"Kwa kutumia jiko hili maana yake huhitaji kutafuta mkaa wala kuni, hivyo kuokoa misitu ambayo inateketea kila siku kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutafuta nishati ya kupikia," anaongeza.

Farida, ambaye pamoja na akinamama wengine 14 – wakiwemo wanahabari watano wanawake – walipatiwa mafunzo ya takriban miezi miwili jijini Madrid, Hispania mapema mwaka huu wa 2016, anasema kwamba lengo la kubuni na kutengeneza jiko hilo la umeme-jua ni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupambana na uharibifu wa mazingira.

Anaeleza kwamba, haikuwa kazi rahisi kwake kukamilisha ubunifu wake, wazo ambalo aliliwasilisha akiwa mafunzoni, na kwamba ndiyo maana mradi wake umechelewa kutokana na kuhitaji teknolojia zaidi.

"Tumeanzisha huu mradi baada ya kukaa na akinamama wa TAWOCA na kuwauliza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maisha yao, moja ya changamoto ni upatikanaji wa kuni na mkaa, gesi na umeme.

"Kwahiyo tukaangalia kama kuna njia mbadala ambayo akinamama wanaweza kuitumia na ikawa nafuu na pia kiafya, kwa sababu njia ya kutumia umeme-jua ina manufaa sana kiafya, kwa hiyo tukaungana na wenzetu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini, CAMARTEC, kwa sababu ndio watafiti wa mashine na zana za kilimo, ili kutengeneza jiko hili linalotumia nishati ya jua," anasema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi anasema imekuwa ni fursa kubwa kwao kufanya kazi na mradi wa Green Voices, kwani wameweza kutengeneza kwa mara ya kwanza jiko hilo ambalo limewapa hamasa wahandisi wa kituo hicho kuliboresha zaidi kwani linaonekana kuwa na manufaa makubwa.

Anakiri kwamba, ingawa wanabuni teknolojia mbalimbali ikiwemo kutengeneza majiko na makaushio yanayotumia umeme-jua, lakini hiyo ndiyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kutengeneza jiko linalotumia nguvu ya jua moja kwa moja.

"Hivi sasa tunafanya utafiti kama tunaweza kulitengeneza dogo lakini lenye nguvu au kutengeneza jiko linaloweza kukunjwa na kuhifadhiwa kirahisi kwa sababu hili ni kubwa na inakuwa shida ikiwa mtu hana nafasi kubwa ya kuhifadhia," anasema Mhandisi Noela.

Akizungumzia kuhusu ufanisi wake, Noela anasema kwamba, jiko hilo ni rafiki mkubwa wa mazingira na lina uwezo mkubwa wa kupika na hata kuoka vyakula vya aina zote ikiwa tu kutakuwepo na jua la kutosha.

Kwa maeneo kame na yenye jua kali kama mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na hata Dar es Salaam, jiko hilo linafaa sana kutumiwa bila shida, anaongeza mhandisi huyo.

Aidha, anafafanua kwamba, jiko hilo linaweza kupika chakula kwa ajili ya watu wengi na kwamba ni jukumu la jamii kugeukia matumizi ya jiko hilo lisilotumia mafuta wala nishati nyingine kwa sababu siyo tu linapunguza gharama, lakini pia linaokoa misitu kwa vile miti haitakatwa ikiwa watakuwa wanalitumia.

"Jambo jingine la muhimu ni kwamba, upikaji kwa kutumia jiko la umeme-jua mara nyingi hufanyika nje na katika mazingira ambayo yanahitaji matumizi madogo ya mafuta na kuni, au hatari ya ajali za moto na inaokoa afya za wanajamii, hususan akinamama pamoja na kuyalinda mazingira yetu," anaongeza Mhandisi Noela.

"Kama unavyoliona, jiko hili limetengenezwa kwa vifaa maalum vikiwemo vioo, ambavyo vinang’aa na kuakisi mwanga wa jua, vimepangwa kitaalam na mwanga huu unapoakisiwa unakwenda moja kwa moja kwenye sufuria ambayo kutokana na joto lake, chakula chochote kinachopikwa kinaiva bila wasiwasi wowote. Kama jua litakuwepo la kutosha, joto linalozalishwa na jiko hili linaweza kufikia hadi nyuzijoto 400 °C."

Kwa mujibu wa mhandisi huyo, vyakula vinavyopikwa kwa kutumia jiko la aina hiyo ni vyema vikawa katika maumbile madogo ili kusaidia kuiva haraka na kwamba muda wa chakula kuiva unategemea na vifaa unavyotumia, kiwango cha jua, na kiasi cha chakula kinachopikwa.

Faida kubwa za utumiaji wa jiko la umeme-jua zinatajwa kwamba, mbali ya kuokoa mazingira, ni uwezo wa kupika vyakula vigumu, kukaanga nyama, kupika supu, kuoka mikate na kuchemsha maji kwa muda mfupi.

Hata hivyo, jiko hilo linahitaji zaidi uwepo wa jua, kwani ndiyo chanzo cha joto linalofaa kupikia.

Mmoja wa wanakikundi hicho, Esther Moshi, amesema kupatikana kwa jiko hilo kutawakomboa wanawake wengi ambao mara nyingi ndio wanaokabiliwa na changamoto ya utafutaji wa nishati za kupikia kama kuni na mkaa.

"Tunashukuru mradi wa Green Voices kwa sababu unalenga kumkomboa mwanamke kutokana na adha ya upatikanaji wa nishati ya kupikia, kama majiko haya yatatengenezwa kwa wingi na kila familia kulipata, hakika yatakuwa mkombozi na yatasaidia kuokoa mazingira, " anasema.

Fatima Aziz Faraji ni mwenyekiti wa Chama cha TAWOCA, amesema ni muhimu kwa wanawake kuzidisha umoja wa vikundi ili waweze kusonga mbele na akaupongeza mradi huo kwamba utakuwa mkombozi si kwa wanawake pekee, bali jamii nzima.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko hilo, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, ameupongeza mradi wa Green Voices pamoja na akinamama hao na akahimiza kuwa, ni vyema kutumia teknolojia ambazo ni rafiki wa mazingira.

Amesema akinamama ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya nishati za kupikia, na kwamba ndio wanaoongoza kupata madhara kiafya, hasa wanapotumia mkaa na kuni.

"Jitihada hizi za wenzetu wa Green Voices zinapaswa kuongezwa, kwa sababu zinalengo siyo tu kumkomboa mwanamke, bali kulinda mazingira yetu ambayo yanazidi kuteketea kila uchao kutokana na ukataji wa misitu kwa madhumuni ya kutafuta kuni na mkaa.

"Akinamama wanaathirika sana, wengine utakuta macho mekundu kutokana na moshi wa kuni, na wanapokuwa wazee ndio wanaoshambuliwa na watu wengine wasio na utu kwamba eti ni wachawi kwa sababu macho yao ni mekundu, lazima kutumia teknolojia mbadala kuwanusuru mama zetu, " alisema.

Hata hivyo, aliwataka akinamama hao kushikamana pamoja katika shughuli zao ili waweze kujiletea maendeleo, kwani umoja ni nguvu.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Green Voices Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, amesema, mradi wa jiko la umeme-jua ni sehemu ya miradi 10 inayotekelezwa chini ya Green Voices ambapo Tanzania ndiyo pekee iliyopendekezwa kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na Taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika, , ambayo inaongozwa na makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandez de la Vega Sanz.

Hata hivyo, taasisi hiyo inafadhili miradi 15 ya wanawake katika nchi 12 barani Afrika ambayo imeonyesha mafanikio, huku mradi wa Green Voices ukitajwa kuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi.

Kwa mujibu wa Bi. Secelela, Mradi wa Green Voices unatekelezwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kigoma, Morogoro na Kilimanjaro.

“Miradi hiyo ni kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani, ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro, usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga, na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi huu wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanjaro,” anafafanua Secelela.

Anasema, lengo kubwa la mradi wa Green Voices ni kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Serikali kupitia taasisi na idara zake zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikiendesha program mbalimbali za mafunzo ya ufundi ikiwemo utengenezaji wa majiko banifu na sanifu kama inayoendelea katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Hata hivyo, bajeti ndogo imekuwa changamoto kubwa kukwamisha kuwafikia wananchi wengi na kuwapatia elimu ya aina hiyo.

SAFARI YA MWISHO YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KATIKA KITUO CHA KIBO KABLA YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU.

Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza .
Safari ilivyoendelea hali ya hewa ilibadirika arikadhalika uoto wa misitu mifupi ulianza kutoweka kadri safari ilivyoenedelea.
Safari iliendelea kwa motto wa "Mdogo Mdogo".
Wakati mwingine kulihitajika maneno ya faraja ili kufanikisha safari hii.

Eneo hili ndilo la mwisho katika Mlima Kilimanjaro kuona maji yakitiririka wakati wa safafri ya kupanda Mlima Kilimnjaro.
Kutokana na kubadirika kwa hali ya hewa ,washiriki wengine walivalia vizuia upepo,wenyewe walivipa jina "Shilawadu".
Baadae uoto wa misitu ukatoweka kabisa ,safari ikawa ni ya kupita katika eneo la jangwa likijulikana kama Saddle.
Safari iliendelea ya kufika kituo cha mwisho cha Kibo Hut.
Wenye kuhitaji Msaada ,walipata msaada.
Mapumziko kwa ajili ya kupata Chakula yalifanyika katika eneo la Saddle.
Safari iliendelea ikiambatana na mvua katika eneo la Jiwe la Okoyo.
Hatimaye Safari ya kutoka kituo cha Horombo ikafikia tamati katika kituo cha Kibo Huts.
Washiriki wakapata picha ya pamoja kabla ya kupata mapumziko kujiandaa na sfari ya kuelekea Kileleni itakayofanyika majira ya saa 5 usiku.
 
Na  Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.

MWANDISHI WA HABARI WA ITV NA REDIO ONE AKITOKA KATIKA KITUO CHA POLISI BAADA YA KUPEWA DHAMANA

Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One Khalfan Liundi (Mwenye shati jeupe) akitoka katika kituo cha Polisi cha Usariver Mara baada ya kupata dhamana,alikamatwa kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti kwa kutuhumiwa kuandika habari za uchochezi picha na mahmoud ahmad waglobu ya jamii arusha

RAIS DKT MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAMTEMBELEA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO

polc1
Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kufuatia kifo cha dada yake nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
polc2
Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbwani kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
polc3Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016 polc4
PICHA NA IKULU