TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu na ajali za barabarani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya kifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 10:00 Asubuhi huko Maeneo ya Kadege, Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za usajili T.913 BEW aina ya Toyota Ipsum iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye MUGANIZI RAPHAEL [34] Mkazi wa Simike iligongana na gari yenye namba za usajili T.204 CSZ/T.670 BEZ aina ya Scania Lory ikiendeshwa na HOSEA S/O MWASHAMBWA [28] Mkazi wa Uyole na kusababisha kifo kwa dereva wa Gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum hasa ukizingatia eneo hilo ni lenye mteremko mkali. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva wa lori alikimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Upelelezi unaendelea.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata hivyo Kumekuwa na matukio 02 ya mauaji kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 25.11.2017 majira ya saa 22:06 usiku huko katika Kijiji cha Ipwizi, Kata ya Mjele, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MINZA PAUL [25] Mkazi wa Ipwizi alifariki dunia baada ya kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina SHILONDI MAKWENGE ambaye alitoroka baada ya tukio.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya mume wa marehemu kurudi nyumbani akiwa amelewa kwa usafiri wa Pikipiki na kumwambia mke wake amlipe pesa dereva bodaboda aliyemlita nyumbani lakini mke wake alimjibu kuwa hana fedha na ndipo SHILONDI MAKWENGE alianza kumpiga mke wake na kusababisha kifo chake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi kwa uchunguzi wa kitabibu. Jitihada za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 15:00 Alasiri huko Mtaa wa Itumbi uliopo Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja mkazi wa Itumbi aliyetambulika kwa jina la FLORIAN KAGOMBE [46] aliuawa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu butu na walinzi wa kampuni ya “Itumbi Reaching Plant” ambao ni 1. IMANI KAYUNI [36] Mlinzi – Panic Security Group na 2. KELVIN NGONYANI [32] Mlinzi – Panic Security Group.

Inadaiwa kuwa, kabla ya kifo chake marehemu alikutwa na walinzi hao eneo la Kampuni ya “Itumbi Reaching Plant” inayojishughulisha na uchenjuaji dhahabu majira ya saa 02.00 usiku na kutiliwa shaka kuwa ni mhalifu/mwizi na hivyo kuanza kumpiga na kumwachia akiwa tabani.

Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa na uplelelezi unaendelea. Aidha mwili wa marehemu umehifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.


TAARIFA YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA IBIGHI, WILAYA YA RUNGWE.

Mnamo tarehe 26.11.2017 kumefanyika zoezi la uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya udiwani. Kwa hapa Mkoa wa Mbeya, zoezi hili limefanyika katika Kata ya Ibighi Wilaya ya Rungwe ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikigombaniwa na wagombea watano.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi kata ya ibighi ndugu STEVEN STANFORD MWAKINGWE ambaye pia ni Afisa Mtendaji Kata ya Ibighi alisema, Jumla ya watu waliotarajia kupiga kura katika kata hiyo ni 4,737 jumla ya vituo vya kupigia kura vilikuwa 13. Idadi halisi ya watu waliopiga kura ni 2,691, kura halali 2,672 na kura zilizoharibika ni 19.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:- 
CCM: SUMA IKENDA FYANDOMO – Kura 1,205 
CHADEMA: SIMBA LUSUBILO EMANUEL – Kura 1,449 
CUF: GRACE NGALABA – Kura 12 
UDP: GEOFREY MWAKAJINGA – Kura 02 
DP: EMANUEL ANDONGOLILE MWAFILAMBO – Kura 0. 

Kutokana na matukio hayo, Msimamizi wa Uchaguzi ndugu STEVEN STANFORD MWAKINGWE alimtangaza rasmi SIMBA LUSUBILO EMANUEL kuwa mshindi na Diwani wa Kata ya Ibighi.
Katika zoezi hilo, hali ya ulinzi na usalama iliimarishwa na zoezi la uchaguzi lilifanyika kwa hali ya amani na utulivu.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio la ajali azitoe ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. 

Pia Kamanda MPINGA anatoa wito kwa madereva kuwa makini ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika. Aidha Kamanda MPINGA anaendelea kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za mtu/watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na wahamiaji haramu kwa hatua zaidi za kisheria.


[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

NBC NA SANLAM WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO


 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya NBC na Kampuni ya Bima ya Sanlam, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka na kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake ndani ya matawi ya NBC nchini kote Waliosisima kutoka kushoto ni, Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. 

 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakifurahi baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika ya benki hiyo na Kampuni ya Bima ya Sanlam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General, Manasseh Kawoloka na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life, Khamis Suleiman. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam General, Manasseh Kawoloka (kushoto), akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya NBC na Sanlam. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakifurahi baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote

 Ni furaha tu baada ya Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), kusaini  mkataba wa ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya benki hiyo na Kampuni ya Bima ya Sanlam, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawokol na kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake ndani ya matawi ya NBC nchini kote Waliosisima kutoka kushoto ni, Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakipiga picha baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano. Wa pili kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.

RC Wangabo Ameitaka Manispaa Ya Sumbawanga kuboresha Masoko

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Matola katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa samaki wa soko la Sabasaba katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la OTC Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akinunua bidhaa alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.


………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanaboresha mazingira ya masoko yaliyopo kwenye Manispaa hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwenye maeneo hayo bila ya kulazimika kufika katikati ya mji kupata huduma hiyo.

Amesema kuwa wakuu wa idara katika Manispaa hawanabudi kuhakikisha wanashuka kuwafuata wananchi na wafanyabiashara wa masoko hayo na kusikiliza kero zao na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya masoko hayo ikiwemo majengo, usafi wa mazingira na vyoo.

“Nimeambiwa changamoto nyingi sana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba na wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira machafu hali ambayo haizoeleki na haifai kuendelea kuwepo, hivyo manispaa lazima iweke kambi kusikiliza kero zao na kuzitatua, kwani lipo kwenye uwezo wao,” Mh. Wangabo alisisitiza.

Aidha, ameitaka manispaa hiyo kuhakikisha usalama wa biashara za wafanyabiashara hao unaimarika ili kupunguza malalamiko yao na kuongeza kuwa atahakikisha malalamiko hayo yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Akielezea changamoto za soko la sabasaba, Mwenyekiti wa soko hilo Feston Mwilema amesema kuwa changamoto kubwa ya soko hilo ni usalama na kuwa hakuna kituo cha polisi na wala hawana mgambo wa kulinda soko hilo, na kuomba kusafisihiwa mazingira kutokana na uchache wa vifaa vya kuzolea uchafu unaozalishwa katika soko hilo.

“Tumelazimika kuchimba shimo la muda la kutupia uchafu unaozalishwa na wauza samaki kutoka na kutokuwepo kwa shimo la kisasa, na tuna kontena moja badala ya matatu ambalo huzidiwa na soko kukosa uzio ni jambo linalotoa mwanya kwa vibaka kuendelea na wizi,” Alisema Mwilema.

Mh. Wangabo alitembelea masoko nane yaliyopo kwenye manispaa ya Sumbawanga na kubaini kuwa masoko mengi hayatumiki kwa kukosa miundombinu bora na usimamizi na hatimae wananchi kuanzisha masoko yasiyorasmi na kuhatarisha usalama wa bidhaa zao na usalama wa vyakula kutokana na kuvidandaza chini na kuhatarisha usalama wa wanunuzi.

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 chahitimishwa kwa burudani ya kukata na shoka jijini Dar Es Salaam


Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.

Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

 Ommy Dimpozi akiendelea kuburudisha katika  jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Vanessa Mdee akiwa na dansa wake wakitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika usiku wa jana  viwanja vya leaders.

Fid q akitoa burudani katika jukwaa la Tigo  fiesta jijini Dar es salaam katika kilele chake kilichofanyika katika viwanja vya Leaders.

Mashabiki wa muziki wakifurahia  burudani mbalimbali zilizotolewa katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

Fid Q akiendelea kuburudisha katika Jukwaaa la Tigo Fiesta .


Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa  katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Maua Sama akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders .

Benpol akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana 


Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.

Richie Mavoko akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha tigo fiesta usiku wa kuamkia jana.

Chege Chigunda akipagawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza katika viwanja vya Leaders katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.

AMREF YAZINDUA MRADI WA HAMASA KATIKA UZAZI WA MPANGO KWA MIKOA 24

 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Wanawake, Jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Hamasa na Tiba kwa Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi mkazi wa Amref Health Africa, Dk. Florence Temu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kwa mikoa 24 nchi nzima ili kuweza kusaidia sekta ya Afya kwa msaada wa Serikali ya Uholanzi.
 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka kutoka Wizara ya Afya Wanawake jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa masuala ya afya ya uzazi na mtoto.
 Meneja mradi wa Masuala wa hamasa na Tiba kwa afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Amref Africa, Dk. Sarafina Mkuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki katika Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa msaada wa Serikali ya Uholanzi.
Baadhi ya Wadau walioshiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa  msaada wa Serikali ya Uholanzi.wakiwa katika picha ya pamoja.

Ubalozi wa Norway nchini Tanzania wachangia Milioni 300 Sauti za Busara 2018

Balozi wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi. Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara 2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari. 

Awali Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu. “Sauti za Busara imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Norway inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia katika maendeleio ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika malengo yake nchini Tanzania. 
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.

Ubalozi wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika la Busara Promotions, ili kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii ni pamoja na kusaidia shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka na tunafurahia kwani tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud. Pia akifafanua umuhimu wa tamasha la Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha hilo limekuwa likiunganisha watu wa rika na asili tofauti huku pia likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba na kuleta umoja, Amani na kuimalisha jamii. 

“Tamasha la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia Yusuf Mahmoud. 


Kwa upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara. “Najisikia furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono. 

Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa ujumla. Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad. 


Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa Norway na Busara Promotions.


Balozi huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana mahala pamoja kufurahia. Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia. 

Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland. Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo. Pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao. 

Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

CECAFA SASA YARUDISHA MICHUANO YA CHALENJI, KUANZA NOVEMBA 25-9DEC


Baada ya kupita miaka miwili bila kuchezwa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki, michuano hiyo imerejea tena msimu huu na Tanzania imethibitisha kushiriki.


Nchi wanachama Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amethibitisha kikosi cha kwanza cha ‘Taifa Stars’ kushiriki na matarajio ya kufanya vema michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Novemba 25, 2017 hadi Desemba 9, mwaka huu.

Kidao amesema kwamba uteuzi wa timu za kwanza kwa kila nchi mwanachama wa Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ni makubaliano ya viongozi wa CECAFA waliokutana kwa pamoja huko Sudan, Septemba, mwaka huu.

Kutokana na makubaliano hayo ya kuita timu za kwanza, michuano hiyo itaathiri kidogot ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kuwa wachezaji wengi wanaounda kikosi hicho, wanatoka timu za VPL.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amesema: “Tutakaa kama kamati na kuangalia siku ya Jumatano na Alhamisi baada ya michuano hiyo na kupanga ratiba ya mechi ambazo zitapanguliwa wakati wa michuano ya Chalenji.”

Mbali ya michuano hiyo, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakayofanyika Bujumbura nchini Burundi kuanzia Desemba 12, 2017 hadi Desemba 22, mwaka huu.

Kadhalika, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji kwa wanawake ikienda kutetea taji katika michuano itakayofanyika Rwanda mwezi Desemba, mwaka huu. Tarehe rasmi itatajwa baadaye.

CECAFA imeamua kurejesha hadhi yake kwani mara baada ya michuano ya Chalenji ya vijana huko Burundi, mwakani itakuwa ni zamu ya Tanzania ambako michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 11, 2018 hadi Agosti 25, mwakani.

Wakati huo huo Kidao amethibitisha Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Chalenji ya CECAFA/CAF kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani na mashindano hayo yatatumika kama sehemu ya kufanya maandalizi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON – U17).

Michuano ya mwakani ina baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa sababu shirikisho hilo linataka kutumia michuano hiyo ya vijana ya Kanda mbalimbali za Afrika kupata timu saba katika michuano AFCON – U17 ya mwaka 2019.


Kanda hizo ni CECAFA (Afrika Mashariki), COSAFA (Nchi za Kusini mwa Afrika), WAFU – UFOA (Afrika Magharibi); UNAF (Afrika Kaskazini) na UNIFFAC (Afrika ya Kati).