CHRAGG yawapiga msasa Waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya haki za binadamu.


Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa, Chitralekha Massey akiwapiga msasa baadhi ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. James Jesse akitoa mada mbele ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.


Afisa Utetezi na Haki za Binadamu wa Shirika la Under The Same Sun (UTSS) Bi. Perpetua Senkoro akitoa mada kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu kupewa haki zao wakati warsha ya siku moja kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.




Wadau wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa Habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja ya warsha kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.

(Picha zote na Benedict Liwenga)


Na Benedict Liwenga.

Asasi za Kiraia pamoja na Taasisi za kutetea haki za binadamu nchini zimewaasa Waandishi wa Habari nchini kujikita katika kuhabarisha umma kuhusiana na masuala ya haki za binadamu ikiwemo mauaji ya watu wenye ualbino, mauaji ya vikongwe, ukatili dhidi ya watoto, pamoja na adhabu ya vifo.

Rai hiyo imetolewa leo na Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika mkoani Morogoro yenye lengo la kuwajengea uelewa Wanahabri kuhusu Mpango wa Kimataifa wa kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR).

Bi. Salma ameeleza kuwa kutokana na tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini, vyombo vya habari havinabudi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa kuziongelea haki za binadamu kwani jamii imekuwa haizitambui baadhi ya haki hizo na kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino, vikongwe pamoja na ukatili kwa watoto.

Ameongeza kuwa, baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kuua watu ambapo watu wenye kuyasemea hayo ni Vyombo vya Habari lengo likiwa ni kukemea kuendelea kwa vitendo hivyo.

“Uvunjaji wa haki za binadamu unafanywa na watu katika jamii, kwa mfano, mauaji ya Watu wenye Ualbino, mauaji ya vikongwe, pale sio Serikali inakua imevunja haki za binadamu, bali ni watu katika jamii”, alisema Bi. Salma.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bi. Chitralekha Massey ameeleza kuwa, ni vema Tanzania ikakubalina na mapendekezo yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu yanayoendana na Dunia kwa ajili ya ulinzi wa haki hizo.

“Sisi kama Umoja wa Mataifa tunapenda kuona Tanzania inafanya uamuzi utakaosaidia kuboreshwa kwa haki za binadamu nchini kwani ni wakati sasa wa jamii kusema kwa uwazi kuwa mapendekezo hayo yatakuwa yenye manufaa kwao”, alisema Massey.

Aidha, katika warsha hiyo, vyombo vya habari, jamii pamoja na Serikali wanajukumu la kulinda haki za binadamu na kuendelea kukemea matukio yanayovunja amani katika jamii.

Tarehe 9 Mei, 2016 Tanzania inatarajiwa kufanyiwa tathmini ya pili juu ya hali ya haki za binadamu nchini na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo tayari Asasi za Kiraia na Watetezi wa haki za binadamu wamekwisha wasilisha mapendekezo yao kwa Wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo.

HOSPITALI ZATAKIWA KUWALINDA WAPOKEA KUMBUKUMBU NA MAAMBUKIZI

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufunga mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi.
                                                                                                             Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao.

Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo, Dk. Mohamed A. Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) zilizofanyika juzi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Mohamed alisema wizara hiyo, inatambua mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi wa kitengo cha kumbukumbu wamekuwa wakifanyia kazi hasa ukizingatia wao ndio watu wa kwanza kukutana na wagonjwa kabla ya kufika kwa madaktari jambo ambalo linaweza kuzua maambukizi kwa magonjwa yaambukizwao kwa njia ya hewa.

“..Natambua pia mazingira mnayofanyia kazi wengi wenu yanayowafanya kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza kwani nyie ndo wa kwanza kabisa kukutana na mgonjwa, kabla ya kuonana na daktari au mtaalamu wa vipimo, hivyo kupata maambukizi ya magonjwa hatarishi hasa yaambukizayo kwa njia ya hewa na mengineyo ni rahisi. Woizara yangu inapenda kuwaagiza Wakuu wote wa hospitali nchini kuhakikisha wanarekebisha mazingira mnayofanyia kazi ili kuondoa hali hii,” alisema Dk. Mohamed akimwakilisha waziri wake.

Aidha wizara hiyo pia iliahidi kushughulikia kero ya uhaba na ukosefu wa wafanyakazi wa taaluma ya utunzaji kumbukumbu za afya kwenye vituo vya afya na hospitali hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuzitaka hospitali na vituo hivyo kuajiri watu wenye taaluma halisi ya utunzaji kumbukumbu na kuhakikisha kada hiyo inapata muundo, stahili zake na kutambulika kama ilivyo kwa makundi ya kada nyingine.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania, Rehema Mwaipaja akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa THERIA ina umuhimu mkubwa hasa ukizingatia kuwa takwimu sahihi za afya ndio msingi bora kwa huduma kamilifu kwa jamii. Aliongeza kuwa uboreshaji wa hali ya ukusanyaji, uchambuzi na utunzaji wa takwimu sahihi za afya unachangia kuboresha tafiti mbalimbali za afya ambazo ni matunda ya ukuaji na uboreshaji wa huduma kiujumla.

“Nidhahiri kuwa ukuaji wa taaluma ya afya hutegemea sana tafiti mbalimbali zitokanazo na taarifa zilizokusanywa na kutunzwa kikamilifu kazi ambayo ni ya msingi kwa afisa kumbukumbu wa afya mahali popote anapofanya kazi, hayo yote huleta faida kwa wagonjwa, taasisi na kwa wafanyakazi,” alisema Bi. Mwaipaja.

Wanachama wa THERIA kutoka mikoa mbalimbali walikutana kwa siku mbili mfululizo katika wao mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo ulifanya uchaguzi kupata viongozi wapya wa chama hicho.

WAHUDUMU WAKIKE WAIVURUGA NDOA YA RYAN GIGGS NA STACEY

Mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs ametengana na mkewe Stacey, na kunamadai kuwa wanatarajia kuivunja rasmi ndoa yao.

Wawili hao walionekana kwenye sherehe pamoja miezi mitatu iliyopita na kwa sasa bado Giggs na Stacey wanaishi kwenye nyumba moja.

Winga huyo wa zamani wa Manchester united, anatuhumiwa kuwa na mahusiano na wahudumu wakike wa hoteli yake anayoimiliki, Jijini Manchester.

Hii si mara ya kwanza kwa Giggs kuchepuka kwani aliwahi kuchepuka na mke wa mdogo wake wa kiume Rhodri aitwae Natasha Lever kwa miaka nane, pia na mwanamitindo Imogen Thomas.

WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA MWILI WAFARIKI DUNIA MJINI MOMBASA

Watoto mapacha walioungana mwili waliozaliwa hospitali ya rufaa ya Pwani mjini Mombasa nchini Kenya wamefariki dunia leo alfajiri.

Watoto hao walizaliwa Alhamisi na walikuwa wasafirishwe kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa ya Kenyatta kwa matibabu maalum wamefariki wakiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Akithibitisha vifo vya mapacha hao Mtendaji Mkuu CPGH Dk. Iqbal Khandwalla ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kwamba jitihada za madaktari za kuokoa maisha ya watoto hao zimeshindikana.

NCCR, CUF NA TLP VIKO ICU SHAKA ALONGA

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapokea kadi ya chadema na kumkabidhi ya CCM alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Kisimani kupitia Tiketi ya chadema Amani John Mgonja Mara baada ya kuhamia Ccm.

                                                                                           Na Mahmoud Ahmad, Kilimanjaro

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umesema muda mfupi ujao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi (CUF ) kwa sababu kimejidhuru kukubali kukumbatia mafisadi .

Aidha umoja huo umevitaja vyama hivyo sasa vinachechemea, vinaishi kwa matimaini na viko mahututi kwani wakati wowote , ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo utakishambiulia chadema.

Matamshi hayo yametamkwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wanachama wa Uvccm na jumuiya zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Maendeleo Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi vijijini.

Shaka alisema jeuri na mbwembwe za NCCR 'Mgeuzi, CUF na TLP muda umepita na sasa havina mategemeao tena ya kuibuka na kushindana na chama tawala .

Alisema vyama hivyo hupenda kujiita vyama vya siasa jambo ambalo alisema si kweli kwasababu kujiendesha kwake kunamtegemea mtu badala ya kujijenga na kuwa taasisi kamili.

Alisema vyama hivyo vineajua kutegemea makapi yaloachwa na ccm ili yawasaidie kuendesha masuala ya kisiasa .

Shaka akizungimza katika mkutano huo alimtolea mfano mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu (chadema) akisema hana uwezo wala uaminifu katika dhima ya kuwatumikia wananchi kwasababu historia yake ya kisiasa haionyeshi kama mtu madhubuti na mwenye msimamo.

"Komu alikuwa mwanachama na kiongozi wa NCCR -Mageuzi tokea mwaka 1992 , akahama na kujiunga Chadema akivutiwa na ukabila, wakati fulani akataka aende TLP Mrema akamuwekea ngumu , aina ya kiongozi kama Komu ni ushahidi tosha si kiongozi muaminifu , kesho sivajabu ukasikia amegama chadema kurudi ccm "alisems Shaka

Hata hivyo Kaimu huyo katibu Mkuu aliitaka halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini kufanya kila linalowezekana kupekeka maji katika maeneo ya kata ya Mabogini ili wananchi waondokane na adha ya ukosefu maji.


"Wananchi wa Moshi vijijini nakuhalikishieni kuwa ujenzi wa barabara yenu umbali wa kilomita 14 toka TPC hadi Chekereni itatekelezwa na serekali ya Dk Magufuli kwa kiwango cha lami "alisema shaka.

Katika kijiji cha Chekereni kata ya mabogini wanachama wapya 34 wamejiunga na Uvccm, 27 CCM na UWT wanachama 12.

MLIPUKO WAUWA AFISA POLISI MMOJA NA KUJERUHI WENGINE 19 NCHINI UTURUKI

Afisa polisi mmoja ameuwawa kwa mlipuko uliokuwa ndani ya gari karibu na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kusini mashariki mwa mji wa Gaziantep nchini Uturuki.

Maafisa polisi 19 na raia wanne wameripotiwa kujeruhiwa na mlipuko huo uliotokea leo asubuhi.

Uturuki imekuwa ikikumbwa na matukio ya mfululizo ya milipuko tangu mwaka uliopita, inayofanywa na wapiganaji wa Kikurdi na Dola ya Kiislam (IS).

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN ASHIRIKI SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA UKUMBI WA SALAMA BWAWANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Wafanyakazi wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) na bango lao linalotoa ujumbe"IDARA YA FIDIA NI UTI WA MGONGO WA MAISHA YA WAFANYAKAZI NI MUHIMU KUANZISHWA" wakati alipokuwa akipokea maandamano ya Wafanyakazi wa Taasisi mballi mbali za Serikali na Binafsi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
Wafanyakazi wakimpungia mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) wakati alipokuwa akipokea maandamano ya Wafanyakazi wa Taasisi mballi mbali za Serikali na Binafsi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja, mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakinyanyua mikono juu kuashiria Mshikamano wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani,ambazo sherehe zimewajumuisha mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Musssa Yussuf wa ZSSF Laki Sitafedha taslim akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZAFICOWV katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Bi.Asya Rajab Said fedha taslim laki tano,kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZUPHE katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Nd,Yunus Sose Hassan fedha taslim laki tano kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZUPHE katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha siku ya Wafayakazi Duniani sherehe zilizofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha siku ya Wafayakazi Duniani sherehe zilizofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.Picha na Ikulu.