NCCR, CUF NA TLP VIKO ICU SHAKA ALONGA

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapokea kadi ya chadema na kumkabidhi ya CCM alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Kisimani kupitia Tiketi ya chadema Amani John Mgonja Mara baada ya kuhamia Ccm.

                                                                                           Na Mahmoud Ahmad, Kilimanjaro

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umesema muda mfupi ujao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi (CUF ) kwa sababu kimejidhuru kukubali kukumbatia mafisadi .

Aidha umoja huo umevitaja vyama hivyo sasa vinachechemea, vinaishi kwa matimaini na viko mahututi kwani wakati wowote , ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo utakishambiulia chadema.

Matamshi hayo yametamkwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wanachama wa Uvccm na jumuiya zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Maendeleo Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi vijijini.

Shaka alisema jeuri na mbwembwe za NCCR 'Mgeuzi, CUF na TLP muda umepita na sasa havina mategemeao tena ya kuibuka na kushindana na chama tawala .

Alisema vyama hivyo hupenda kujiita vyama vya siasa jambo ambalo alisema si kweli kwasababu kujiendesha kwake kunamtegemea mtu badala ya kujijenga na kuwa taasisi kamili.

Alisema vyama hivyo vineajua kutegemea makapi yaloachwa na ccm ili yawasaidie kuendesha masuala ya kisiasa .

Shaka akizungimza katika mkutano huo alimtolea mfano mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu (chadema) akisema hana uwezo wala uaminifu katika dhima ya kuwatumikia wananchi kwasababu historia yake ya kisiasa haionyeshi kama mtu madhubuti na mwenye msimamo.

"Komu alikuwa mwanachama na kiongozi wa NCCR -Mageuzi tokea mwaka 1992 , akahama na kujiunga Chadema akivutiwa na ukabila, wakati fulani akataka aende TLP Mrema akamuwekea ngumu , aina ya kiongozi kama Komu ni ushahidi tosha si kiongozi muaminifu , kesho sivajabu ukasikia amegama chadema kurudi ccm "alisems Shaka

Hata hivyo Kaimu huyo katibu Mkuu aliitaka halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini kufanya kila linalowezekana kupekeka maji katika maeneo ya kata ya Mabogini ili wananchi waondokane na adha ya ukosefu maji.


"Wananchi wa Moshi vijijini nakuhalikishieni kuwa ujenzi wa barabara yenu umbali wa kilomita 14 toka TPC hadi Chekereni itatekelezwa na serekali ya Dk Magufuli kwa kiwango cha lami "alisema shaka.

Katika kijiji cha Chekereni kata ya mabogini wanachama wapya 34 wamejiunga na Uvccm, 27 CCM na UWT wanachama 12.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni