Fundi ujenzi mmoja huko Bristol
nchini Uingereza, ameokolewa maisha yake na muuguzi ambaye aliyekuwa
mapumzikoni baada ya kuchomwa kisu na kuachwa mtaani akingojea kifo
chake.
Picha za tukio hilo la kutisha
zinamuonyesha mtu aliyetapakaa damu akiwa amelala chali chini huku
muuguzi huyo mwanamke akiwa amepiga magoti na kumsaidia kupumua mtu
huyo ambaye alishaanza kukata pumzi.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema
fundi huyo mwenye miaka 41, alianza kuishiwa na pumzi na mwili wake
ulikuwa umeshalegea, hata hivyo muuguzi huyo alimsaidia hadi
kilipokuja kikosi msaada wa dharura chenye vifaa tiba.
Muuguzi wa kike akimsaidia kupumua mtu aliyechomwa kisu
Watu wa huduma ya kwanza wakiwa wamefika na kuanza kutoa huduma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni