![]()  | 
| Haji Kihwele kutoka shirika la Oxfam akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida. | 
![]()  | 
| kurugenzi wa SHIDEPHA+ Venance Muzuka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida. | 
![]()  | 
| Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila. | 
![]()  | 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Josephine Matiro  | 
![]()  | 
| Wakazi wa kijiji cha Nyida wakiangalia hati zao walizopokea. | 
![]()  | 
| Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila. | 
MKUU
 wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amekabidhi jumla ya hati za 
hakimiliki za kimila 92 kwa wakazi wa kijiji cha Nyida mkoani Shinyanga.
Hatua
 hiyo ya ugawaji wa hati ilifanyika hivi karibuni katika Wilaya hiyo, 
baada ya viwanja vya wakazi hao kupimwa na kupatiwa mafunzo ya matumizi 
bora ya ardhi.
Alisema
 Hati hizo zitawasaidia wananchi kupunguza au kuondoa kabisa migogoro ya
 ardhi katika wilaya hiyo kwa sababu watakuwa wanamiliki maeneo yao 
kisheria.
Matiro
 alisema migogoro mingi ya ardhi inatokea kutokana na watu kutokuwa na 
hati zinazoonyesha ukubwa wa maeneo yao na kusababisha mgogoro baina ya 
mtu na mtu.
Matiro
 aliwapongeza maafisa ardhi kwa kuweza kufanya kazi hiyo kwa kutumia 
shilingi milioni tatu kwa kila kijiji tofauti na milioni tisa 
iliyoelekezwa na serikali.
“Natoa
 shukrani zangu za dhati  kwa ushirikiano mkubwa na ufadhili kutoka kwa 
wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Oxfam na SHIDEPHA+ kwa kusaidia 
kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi ili wananchi wa wilaya yangu 
kufahamu umuhimu wa hati hizo,” alisema.
Kwa
 Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,
 Kiomoni Kibamba alisema kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Oxfam na
 SHIDEPHA+ wamefanikiwa kutekeleza mradi wa kuandaa mpango wa matumizi 
bora ya ardhi ndani ya vijiji vinne ambavyo ni Shabuluba, Nyida, Mwenge 
na Puni.
Alisema mradi huo ulianza mwezi wa Februari 2016 na sasa upo katika hatua za mwisho za utekelezaji katika vijiji hivyo.
Alitaja
 changamoto mbalimbali  za kupata haki miliki za kimila kuwa ni pamoja 
na ukosefu wa rasilimali fedha ndani ya jamii, baadhi ya wananchi 
kugubikwa na umaskini na kukosa fedha kwa ajili ya kuchangia gharama za 
upimaji.
Kibamba
 alisema changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa vigezo elekezi 
vya Wizara na kanuni ya sheria ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 kuhusu 
kupatiwa hati miliki ndani ya serikali za vijiji ambavyo ni pamoja na 
kukosa ofisi zenye hadhi za Halmashari za vijiji pamoja na ukosefu wa 
masijala za ardhi na daftari za ardhi za vijiji kwa ajili ya usajili wa 
Hakimiliki za kimila.
“Faida zilizotokana na mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi
 katika halmashauri ni pamoja na uhamasishaji na utoaji wa elimu juu ya 
hati za haki miliki za kimila uliotolewa kwa vijiji vinne pamoja na 
kupunguza na kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi ndani ya jamii katika 
vijiji husika,” alisema Kibamba.
Alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira kwa 
kupanga matumizi sahihi ya ardhi ndani ya mipaka ya kijiji, umiliki wa 
ardhi kisheria ndani ya jamii kwa wananchi kupatiwa hati za hakimiliki 
za kimila pamoja na jamii kupata uwezesho wa kifedha kutoka taasisi za 
kifedha baada ya kupatiwa hati miliki.
Nae miongoni mwa wakazi waliopokea hati hizo ambae ni  Mkazi wa Kijiji 
cha Nyida, Flora Nkingwa alishukuru kukabidhiwa hati hizo kwani sasa 
anamiliki eneo lake kisheria.
Nkingwa alisema eneo alilopatiwa hati lina ukubwa wa nusu ekari ambalo analitumia kwa kilimo cha Mahindi na Karanga.
Hati hizo za bila kikomo zilitolewa kwa mchanganuo wa hati 75 za 
familia, hati 7 za wanawake, hati 5 za wanaume, hati 2 za Taasisi na 
hati 3 za ukoo.











Hakuna maoni:
Chapisha Maoni