Jiji la Bujumbura linavyoonekana katika picha.
………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Vyama tisa vya upinzani
vilivyoshiriki uchaguzi wa Burundi wa mwaka 2015 na ambavyo
vinashiriki mazungumzo ya kutafuta amani ya Burundi vimetaka wawakilishi
wa umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kutoshiriki katika mazungumzo ya
amani ya Burundi.
Viongozi wa vyama hivyo kwa
pamoja wanasema kuwa wawakilishi wa taasisi hizo wameonyesha kuegemea
upande katika mgogoro wa Burundi kufuatia msimo wao wa kutaka chama cha
CNARED ambayo wanadai imeshiriki katika vurugu na mauaji nchini Burundi
kushiriki katika mazungumzo hayo.
Katika taarifa yao ilitiwa
sahihi na viongozi wote tisa wa vyama hivyo ,wamesema kutokana na
lugha na misimamo ya wawakilishi hao wa taasisi za juu ni wazi
wataharibu mchakato huo unaoendelea wa n kutafuta amani ya Burundi.
Taaarifa iliyotolewa na viongozi
wa vyama hivyo baada ya kumalizika mazungumzo ya awali ,viongozi hao
wamemtaka msuluhishi wa mgogoro huo Rais mstaafu wa Tanzania
kutokukubalina na wawakilishi hao na kushirikisha pande zote zenye
masilahi na mgogoro wa Burundi.
“Tunamtaka msuluhishi alione
hili na kuonya taasisi hizo kuacha propaganda za kuwagawa Warundi
katika mgogoro huo “taaarifa hiyo ilisema .
Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa
Burundi itizamwe kama serikali halali iliyochaguliwa na wananchi na
haipaswi kuingiliwa uhuru wake na watu ama taasisi za nje.
Aidha taarifa hiyo ilivitaja
vyama hivyo kuwa ni UPRONA ,FNL,FNL IRYAGIRAGAHUTU,RADEBU,zingine ni
RADEBU,FLORINA,MSPINKINZO Y’IJAMBO ,PMP,PRP na PIEBU.
Na katika hatua nyingine akifunga
mazungumzo hayo ya awali msuluhishi wa mgogoro huo Rais Benjamen Mkapa
ameeleza kuridhishwa na jinsi wajumbe wa mazungumzo hayo walivyoshiriki
mazungumzo hayo ya awali kwa dhati na kuonyesha nia kutaka amani katika
taifa lao.
“Nimeguswa na namna mlivyoonyesha
katika fikra na mawazo yenu ,mmeonyesha uzalendo mkubwa kwa kuonyesha
madhara ya mgogoro katika nchi yenu kiuchumi na maisha ya watu
yanayoharibiwa na mgogoro huo”Alisema Mkapa .
Mkapa ambaye anafanya usuluhishi
huo chini ya rais Yoweri Mseveni aliyeteuliwa na marais wa Afrika
mashariki kutatua mgogoro alishukuru uwepo uwepo wa taasisi za kimataifa
na za kikanda katika mazungumzo hayo.
Aidha rais Mkapa aliwaambia
wajumbe wa mkutano huo kwa muda wa wiki tatu zijazo atahakikisha kuwa
anafanya mazungumzo na makundi mengine ambayo yalialikwa lakini
hayakuweza kufika Arusha kutoa maoni yao kuhusu utatuzi wa mgogoro wa
nchi yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni