Mkurugenzi
 Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi 
(kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja 
Jenerali Gaudence Milanzi kuelkea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi 
ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya 
waajiriwa wa shirika hilo .
Katibu
 Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride 
maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya  mabadiliko ya mfumo wa 
utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu.
Katibu
 Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu 
mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa 
kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo 
Mlele mkoani Katavi.
Askari
 waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya 
mgeni rasmi (hayupo pichani)  kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati
  ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi 
Katibu
 Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa 
heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya 
Wanyamapori ,Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali 
Mstaafu,Raphael Muhuga,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za 
Taifa,Allan Kijazi,Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori,Ndugu 
Karamaga.
Askari
 waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya 
mgeni rasmi (hayupo pichani)  kwa mwendo wa haraka wakati  ufungaji wa 
mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi 
Askari
 wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha 
umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara 
baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani 
Katavi. 
Baaadhi
 ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada
 ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko
 ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu. 
Askari
 wa Hifadhi akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga 
shabaha wakati wa kuhitimu mafunzo ya  awamu ya kwanza ya mabadiliko ya 
mfumo  wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika 
katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi
Baadhi
 ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa 
Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho 
yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.
Meneja
 Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete 
(kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika 
hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na 
Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .
Mhifadhi
 Sekela Mwangota akisoma risala  ya Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa 
Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na 
Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa 
kuhitimisha mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa 
shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya 
Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Kaimu
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori,Martin Loibooki akizungumza wakati
 wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi 
na Asakari Waajiriwa .
Baadhi ya Wahitimu.
Mkurugenzi
 Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza 
wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa 
Wahifadhi na Askari Waajiriwa .
Mkuu
 wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza 
hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na 
Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji 
kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.
Katibu
 Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa 
Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini 
(TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Baadhi ya Askari Waliohitimu.
Katibu
 Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akitunuku vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa 
Wahifadhi za Taifa(TANAPA) yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani 
Katavi. 
























Hakuna maoni:
Chapisha Maoni