Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Wilson Nkhambaku, ametangaza kubaini na kuwashikilia watumishi hewa 132 ambao wamepatikana kutoka Halmashauri za Arusha na Meru zilizopo kwenye Wilaya hiyo.
Aidha, Nkhambaku amesema bado wanaendelea kuwahoji huku uchunguzi zaidi ukiendelea, na kwambw tayari akaunti zao zimefungwa lengo likiwa ni kudhibiti kutoingiziwa tena fedha.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Arusha, Nkhambaku alisema kati ya hao, 28 wanatoka katika Halmashauri ya Arusha na waliobaki wanatoka Halmashauri ya Meru.
Alisema kufuatia hatua hiyo, tayari Wilaya imesharudisha zaidi ya Sh milioni 70, baada ya watuhumiwa wote kujisalimisha na kurejesha fedha hizo, na kwamba zaidi ya milioni 10 zimepatikana Halmashauri ya Arusha na nyingine Halmashauri ya Meru.
Nkhambuka aliongeza kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa wote watakaobainika watafikidhwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi wa nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni