Kaimu
Muuguzi Mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Flora
Kasembe, (wapili kulia), akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wagonjwa
waliolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha JKCI, wakati Naibu
Balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (wapili kushoto),
alipotembelea kambi ya upasuaji wa moyo iliyoendeshwa na taasisi hiyo
kwa kushirikiana na taasisi ya hiari ya Uinegereza ya Muntada Aid, Mei
3, 2016. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa
Mohammed Y.Janabi, Meneja Mradi wa Muntada Aid, Kabir Miah, Mkuu wa
Upasuaji wa JKCI, Dkt.Peter Kisenge, na Daktari Bingwa wa Moyo wa JKCI,
Dkt.Tulizo Shem
Profesa Janabi (kushoto) na Balozi Sutherland baada ya kutembelea chumba cha Coronary care unit
NA K-VIE MEDIA/Khalfan Said
NAIBU
balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (pichani wapili
kushoto), ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa
kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka
nje kwa mafanikio makubwa.
Pongezi
hizo amezitoa leo May 3, 2016, baada ya kutembelea kambi hiyo maalum
iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na kazi
ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali
nchini.
“Nimefurahishwa
sana na uamuzi wa JKCI wa kuratibu zoezi hili kwa ushirikiano na
wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua taasisi ya hiari
kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na madaktari
wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema Balozi
Sutherland.
Taasisi
ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake nchini
Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na
hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI
wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Janabi alisema, chini ya uratibu wa
taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart
International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi
ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia Aprili 25 hadi Aprili 30.
“Kambi
hii ya sasa, inaundwa na wataalamu kutoka Saudi Arabia chini ya uratibu
wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini Uingereza,
na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa upasuaji
na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi
hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na
waandishi wa habari.
Profesa
Janabi alisema, malengo yao ni kuwafanyia upasuaji watoto 70 Ifikapo
Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana nasi kwani
upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua
mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo
muhimu kwa wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka
kwao.” Alisema.
Profesa Janabi (wapili kulia), wengine kutoka kulia, ni Balozi Sutherland, Dkt. Shem, na Dkt.Delila Kimambo
Balozi Sutherland, katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka JKCI na wale wa Muntada Aid
Profesa Janabi, akimsikiliza mgeni wake, Balozi Sutherland
Dkt.StellaMongella.
(kushoto, akimpatia maelezo Balozi Sutherland, alipotembelea wodi ya
watoto waliofanyiwa upasuaji (Post Operative Recovery Word), Kulia ni
Profesa Janabi.
Balozi
Sutherland, akiwapongeza wataalamu wa moyo kutoka Muntada Aid,
wanaoshuhudia ni Profesa Janabi (kulia na Dkt. Tulizo Shem kutoka JKCI.
Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka Muntada Aid, (katikati)
Dkt. Tulizo Shem akiongea
Balozi Sutherland akipokewa kwenye taasisi alipowasili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni