Mwenyekiti
wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la
Tanzania, Simon Berege, akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika
Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Berege
amesema Maadhimisho hayo yanafanyika huku wanahabari wakiwa wanapitia
manyanyaso kutoka kwa vyombo vya dola, Wanasiasa na wakati mwingine
kutoka kwa wananchi ambapo mwaka jana kuliripotiwa kesi 30 za manyanyaso
kwa waandishi wa habari.
Ametoa
rai kwa Serikali kufuta uamuzi wake wa kuzuia wananchi kupata habari,
kwa kuzuia matangazo ya shughuli za bunge kuonyeshwa moja kwa moja
(Live), huku akivisihi vyombo vya habari vya kijamii kurusha live vikao
vya mabaraza katika halmashauri nchini ili kutoa fursa kwa wananchi
kufuatilia bajeti za halmashauri zao.
Katika
Maadhimisho haya, litazinduliwa Chapisho la Uhuru wa Vyombo vya Habari
Kusini mwa Afrika ambalo limeandaliwa na Misa Tanzania, chapicho hilo
linaitwa "So This is Democracy"? (Je Hii ni Demokrasia).
Mgeni
Rasmi katika Maadhimisho haya ni Jaji Mkuu wa Tanzania ambae
amewakilishwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,
Mhe.Robert Vicent Makaramba.
Pia
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nhauye pamoja
na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Regnard
Mengi wamehudhuria katika Maadhimisho haya.
Viongozi
wengine wa Mashirika ya Kimataifa, Balozi mbalimbali, Taasisi
Washirika, Wasomi wa Vyuo Vikuu pamoja na Wadau wengine wa habari
wamehudhuria.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la
Tanzania akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya
Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Zulmira
Rodrigues ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa UN nchini
Tanzania, akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya
Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Mgeni
rasmi Mhe.Robert Vicent Makaranga (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na
wageni waalikwa wengine katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika
Beach Resort Jijini Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni