Na Benedict Liwenga, Maelezo.
Kiongozi
wa Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler
(1889-1945) alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu
kuwahi kutokea katika karne ya 20.
Baada
ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mbabe huyo aliamka kwa nguvu kupitia
Chama hiko cha Wafanyakazi wa Ujerumani na kuchukua udhibiti wa Serikali
ya Ujerumani mnamo mwaka 1933.
Hitler
aliamuru uanzishwaji wa kambi za mateso dhidi ya Wayahudi na makundi ya
watu wengine huku akiamini kuwa kufanya hivyo ilikuwa chachu na tishio
tosha dhidi ya ukuu wa himaya ya Aryani na hatimaye kusababisha vifo vya
zaidi ya Wayahudi wapatao milioni Sita.
Mashambulizi
ya Ujerumani dhidi ya nchi ya Poland mwaka 1939 ndiyo yaliyoanzisha
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo mpaka kufikia mwaka 1941Ujerumani
iliteka sehemu kubwa ya ardhi ya Ulaya na Afrika Kaskazini.
Ili
kuepuka kukamatwa kwa kukwepa utumishi katika jeshi la Austria-Hungary,
Adolf Hitler aliondoka toka Vienna na kuelekea Munich mnamo Mei 1913
lakinibaadaye alilazimika kurudi tena.
Taarifa
za kihistoria zinasema kuwa Kiongozi huyo wa Nazi alijiunga na jeshi la
Bavaria na kuanza kufanya kazi za kujitolea ambapo mwaka uliofuata
alishiriki kikamilifu katika vita ya Kwanza ya Dunia akiwa mstari wa
mbele upande wa Magharibi ambapo uzoefu wake katika vita na mapambano
uliathiri mawazo, fikra na mitazamo yake yote baada ya hapo.
Baada
ya Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, Hitler alichukua udhibiti wa chama hiko
cha wafanyakazi wa Ujerumani kama kiongozi hivyo alitumaini
kingemwezesha kushika dola ya Ujerumani punde si punde.
Aliposhindwa
kwenye jaribio la Mapinduzi la mwaka 1923 yeye na wenzake walikamatwa
na kufungwa jela na baada ya kutoka jela alijitahidi kukijenga chama
hiko na kuanza mikakati ya kukamata dola kwa njia zilizo halali.
Hitler
alikusudia kufanya mageuzi na kuendesha sera za kibaguzi ambazo
zingetoa nafasi ya kutosha kwa Wajerumani kuweza kuishi katika himaya
kubwa duniani.
Kwanza
alitabiri ingekuwa rahisi kuiteka Czechoslovakia, na kufuatiwa na
Ufaransa ambayo ilikuwa kizingiti kigumu kwa wakati huo hatimaye
kumalizia na nchi ya Uingereza.
Kwa
mujibu wa mikakati ya Adolf Hitler, vita ya Tatu ingefuata juu ya
uvamizi dhidi ya Jumuiya ya Kisovieti ambayo kwake ulikuwa ni mtihani
ambao alipanga afaulu kwa kufikiri vita ingepiganwa kwa haraka na kwa
urahisi.
Kwa
mujibu wa fikra zake za kuipiga Urusi, hii ingempa utajiri wa malighafi
za kutosha hususan mafuta ambayo yangemwezesha kuandaa mkakati wa
maandalizi ya vita ya Nne dhidi ya Marekani.
Vita
hiyo ingekuwa rahisi tu kwake endapo Ujerumani ingeweza kuwa na ndege
ziwezazo kusafiri masafa marefu pamoja na meli za kivita na kwa upande
mwingine ndege za kutosha na jeshi la maji kubwa na imara lingemwezesha
kumkabili adui kokote aliko bila umbali kuwa kikwazo.
Mara
baada ya Hitler kuingia madarakani mwaka 1933, maandalizi ya Ujerumani
kijeshi yalianza kufanyika, hivyo mkazo na mkakati wa muda mfupi ulikuwa
kutengeneza silaha kwa ajili ya vita dhidi ya mataifa ya Magharibi na
mkakati wa muda mrefu ulikuwa juu ya uzalishaji wa silaha nzito kwa
ajili ya vita dhidi ya Marekani.
Mnamo
mwaka 1938 Hitler aliachana na mpango wa uvamizi wa kijeshi dhidi ya
Czechoslovakia na kuangalia zaidi makubaliano ya amani na kiongozi wa
nchi hiyo ambayo yalifanyika mjini Munich na hilo lilikuwa kosa lake
baya na kubwa kuwahi kulifanya.
Alipoamua
kuigeukia Ufaransa na Uingereza Hitler hakuweza kuishawishi Serikali ya
Poland kujiunga na kuwa sehemu ya himaya ya Ujerumani kwa njia za amani
ili kuhakikisha hali ya utulivu inakuwepo katika Mashariki ya Ulaya,
hivyo alichukua maamuzi ya kuivamia na kuiharibu Poland kabla ya kuanza
kuzikabili nchi za Magharibi.
Uvamizi
wa nchi ya Poland ulikususudiwa kufanyika ifikapo Septemba 1, 1939
lakini, ili kufanikisha adhma yake hiyo na ushindi wa haraka juu ya
Poland kwa kuvunja kila aina ya kikwazo mbele yake, alikusudia kuiingiza
Ujerumani katika makubaliano na Urusi ili mwisho wa siku iwe rahisi
kwake kuzivamia nchi za Magharibi bila pingamizi lolote baada ya Poland.
Hali
kadhalika, Hitler alikusudia kufanya uvamizi dhidi ya Mataifa ya
Magharibi katika msimu wa baridi mwishoni mwa mwaka 1939, lakini hali
mbaya ya hewa ilikuwa ni kikwazo kikubwa ambacho kingeathiri jeshi lake
la anga, kwahiyo aliamua kuhairisha mpango huo na kuhamishia uvamizi
huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 1940 katika majira yajoto.
Kutokana
na ushauri alioupata toka kwa Admiral Erich Raeder juu ya kuivamia na
kuiteka Norway ili kuwezesha upatikanaji wa njia rahisi kwa jeshi lake
la maji katika bahari ya Atlantiki kuelekea Kaskazini, aliivamia Norway
mwaka Aprili 1940.
Baada
ya kupokea ushauri tena toka kwa Kamanda Mkuu Erich Von Manstein lengo
la uvamizi kuanzia Kaskazini lilibadilishwa na kuamua kupanga
mashambulizi kuelekea nchi zilizoko Kusini mwa Ulaya kwa lengo la kuzuia
misaada ya kijeshi toka jeshi la Washirika (Allied force) kuelekea nchi
za Ubelgiji na Uholanzi.
Mkakati
mpya wa Hitler kwa mara ya kwanza ulionekana kufanya kazi wakati jeshi
la Ujerumani lilipofanikiwa kuvunja mstari wa ulinzi wa jeshi la
Kifaransa na kufanikiwa ndani ya siku kumi kufika kwenye mkondo wa pwani
nyuma ya vikosi vya majeshi ya Muungano.
Baada
ya kuonekana wazi kuwa majeshi ya Washirika yaliyokwama yanaweza
kutotoroka kipigo cha jeshi la Ujerumani, mwelekeo wa silaha na jeshi la
Ujerumani ulibadilika tena, lakini jeshi hilo lilikwisha chelewa kuweza
kuzuia na kufanya mashambulizi dhidi ya askari wa jeshi la Muungano
kwasababu kikosi maalumu cha jeshi la Uingereza na wanajeshi wa Ufaransa
walifanikiwa kuokolewa na kutoroka.
Pigo
lililotokea mapema mwa mwezi Juni 1940 lililopelekea anguko kwa mstari
wa mwisho wa ulinzi wa jeshi la Ufaransa ulikuwa ni ushindi kamili
uliompa Hitler furaha na shangwe huku akijua anapata msaada wa kutosha
toka kwa Makamanda na Majemedali wake wa kivita, ambao kila mara alikuwa
akiwapandisha vyeo na kuwapa namna nyingine za rushwa kama sehemu ya
kuwapa motisha ya kuendelea na mapambano.
Taarifa
zinasema kuwa, kwasababu ilionekana kama vita hii ilikuwa imeisha baada
ya Ujerumani kuiteka Ufaransa, Hitler alianza kupanga mipango mingine
kwa ajili ya vita dhidi ya Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Mnamo
Julai 11, 1940 Hitler alitoa amri kuanza kwa ujenzi wa jeshi la maji
ikiwemo ujenzi wa meli za kivita na ilipofika Julai 31, 1940 baada ya
mkakati wa kutaka kuvamia Umoja wa Kisovieti katika msimu wa baridi wa
1940, Hitler kutokana na ushauri wa wafanyakazi wake wa kijeshi aliamua
kuishambulia Urusi katika majira ya joto mwishoni mwa mwaka1941.
Wakati
Uingereza ikikataa kukubali kushindwa na kusalimu amri, Hitler alipanga
kuchanganya hatua tatu ambazo zingehakikisha Uingereza inasalimu amri;-
Kwanza kabisa, jeshi la anga la Ujerumani lingefanya uvamizi na
kuharibu uwezo wa Uingereza kujitetea; Pili Uingereza ingevamiwa ardhini
iwapo kama isingejisalimisha, na tatu ushindi ambao ungepatikana dhidi
ya Urusi ungeondoa uwezekano wa Uingereza kupata msaada wowote ule toka
Urusi, hivyo kuangamia zaidi na kumaliza hatari yoyote dhidi ya Japan,
ambayo ingehamasika kusafiri katika bahari ya Pasifiki na kuivamia
Marekani upande wa Magharibi.
Kwa
upande mwingine Hitler alitaka Japan kujiunga katika vita na Uingereza
na kuahidi kujiunga na Japan katika vita dhidi ya Marekani kama Tokyo
ingeona umuhimu juu ya hilo, na hii ingekuwa njia nyingine kwa Ujerumani
kupata kuimarisha jeshi la maji dhidi ya Marekani.
Kampeni
dhidi ya eneo la Balkan, kiongozi huyo mbabe wa enzi hizo (Hitler)
alikusudia kupata alicho amini kuwa ngome ya upande wa Kusini iliyokuwa
katika hali tete lakini hata hivyo aliona operesheni kubwa ya jeshi la
anga katika eneo la Balkani ingekuwa ya gharama ya juu sana kutokana na
ugumu wa eneo lenyewe na hivyo kutokusudia kufanya operesheni kama hiyo
tena.
Ikumbukwe
kuwa, uvamizi wa Ujerumani dhidi ya Umoja wa Kisovieti, ulianza tarehe
22 Juni, 1941 ambapo hapo mwanzo uvamizi huo ulionekana kwenda kama
ilivyo pangwa, lakini gafla kila kitu kilianza kwenda vibaya vipigo vya
kwanza ambavyo vilikusudia kuangusha Umoja wa Kisovieti ndani ya wiki
chache havikuleta matokeo yaliyokusudiwa na hayakuweza kuwa na athari
katika nchi hiyo, hivyo baada ya hapo, swali daima lilikuwa kwa
Ujerumani ni sekta ipi nyeti na muhimu ishambuliwe ili kuidhoofisha
Urusi na sekta gani iachwe.
Katika
hali hiyo, Hitler alijikuta mara kwa mara akitofautiana na Majenerali
wake walioko mstari wa mbele katika kuamua mustakabali wa vita na baada
ya vita kuonekana ikiielemea na kuigeukia Ujerumani hali ya kutofautiana
kati ya Makamanda wa Hitler ilizidi kuongezeka.
Wakati
jeshi la Ujerumani likiendelea kurudi nyuma, Hitler alikuwa daima na
wasiwasi kuhusu hasara waliyokuwa wakiendelea kuipata ya watu hali
kadhalika ya uharibifu wa vifaa vyake vya kijeshi kwahiyo baadhi ya
Majemadari kama Erwin Rommel na Walther Model, mara kwa mara walikuwa
wanapingana na amri ya Hitler kwa kurudi nyuma wakati Majenerali wengine
walikuwa wakirudishwa nyumbani kukusanya kiinua mgongo chao cha kila
mwezi na kustaafu kwa kutofautiana na amri za kiongozi wao ingawa
wengine walikuwa wakiendelea na kazi zao.
Hitler
alifikiri kwamba kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Kuu ya Kwanza ya
Dunia kulitokana na anguko lililotokea katika ardhi ya nyumbani mbele na
kwa hivyo kudhani kuwa uanzishwaji wa sera za kidikteta na mauaji ya
kukusudiwa ya Wayahudi ulikuwa uhakika wa ushindi wa vita dhidi ya
majeshi washirika na safari hii Hitler alipoona hana jinsi na majeshi
washirika yameshaingia mjini Berlin huku yakiongozwa na Jeshi Jekundu la
Urusi, Hitler alijawa na hofu ya kisasi ambacho Warusi wangetoa dhidi
ya Wajerumani, hivyo aliamua kumuoa mke wake na wote kwa pamoja kuamua
kujiua muda mfupi kabla ya jeshi la Urusi kuwasili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni