Ipo
kauli isemayo “Mfupa Uliomshinda Fisi” ikiashiria jambo gumu mithiri ya
mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyama bingwa wa kutafuna
mifupa ya kila aina.
Ndivyo
unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini
Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri
ya jiji la Mwanza.
Mara
kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka
wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya
biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake
umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu
licha ya nguvu kubwa kutumika.
Kabla
ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji
la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi
lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya
ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la
mwanza machinga wamezagaa ovyo.
Baadhi ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni