Kuiba kiasi kidogo cha chakula ili
kujiokoa na njaa si uhalifu, Mahakama ya Juu ya Rufaa nchini Italia
imetoa uamuzi huo.
Majaji wa mahakama hiyo wametengua
hukumu dhidi, Roman Ostriakov, baada ya kuiba jibini na soseji zenye
thamani ya dola 4.50 kwenye duka kubwa la bidhaa.
Mahakama imesema Ostriakov, ambaye
ni raia wa Ukraine asiyena makazi aliiba chakula kwa mahitaji ya mara
moja ya dharura, na ambacho kinahitajika kwa virutubisho vya mwili,
hivyo kitendo hicho sio uhalifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni