Mbunge
wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea
Hospitali ya wilaya ,Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana
na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Wanafunzi
katika shule iliyo jirani na barabara hiyo wakitizama sehemu ya korongo
lililopo katika barabara hiyo ambayo ni tegemeo kwa Chuo cha Ualimu
Mandaka,Seminari ya Mtakatifu James ,shle za sekondari pamoja na msingi.
Baaadhi
ya madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakipita katika barabara
hiyo ambapo kwa sasa nauli ya kupandisha abiria kwenda Hospitali ya
wilaya ya Moshi,Kilima imepanda kutoka kiasi cha sh 3000 hadi 6000 .
Moja
ya Magari yanayotumia barabara hiyo likijaribu kupita katika barabar
hiyo ambayo imeharibika vibaya kutokana na maji yaliyosababishwa na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Sehemu
ya barabara hiyo likionekana korongo ambalo limeanza kumegwa na maji na
kuhatarisha kukatika kwa mawasiliano katika baina ya vijiji 12 ambavyo
wakazi wake wanatumia barabara hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni