Mchezaji nyota wa zamani wa
Manchester United, Ryan Giggs ametengana na mkewe Stacey, na
kunamadai kuwa wanatarajia kuivunja rasmi ndoa yao.
Wawili hao walionekana kwenye
sherehe pamoja miezi mitatu iliyopita na kwa sasa bado Giggs na
Stacey wanaishi kwenye nyumba moja.
Winga huyo wa zamani wa Manchester
united, anatuhumiwa kuwa na mahusiano na wahudumu wakike wa hoteli
yake anayoimiliki, Jijini Manchester.
Hii si mara ya kwanza kwa Giggs
kuchepuka kwani aliwahi kuchepuka na mke wa mdogo wake wa kiume
Rhodri aitwae Natasha Lever kwa miaka nane, pia na mwanamitindo
Imogen Thomas.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni