Waziri
 wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo (katikati waliokaa) 
akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa 
Geita, baadhi ya Wabunge na  Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa
 Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala 
wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa 
(STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Wa 
Pili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel 
Kyunga.
 Waziri
 wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Wa Pili kulia) akiwa na
 baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita, waliohudhuria kikao baina ya 
Waziri na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge
 na  Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na 
Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini 
Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya 
kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Kikao kililenga katika 
kujadili suala la magwangala na maeneo ya wachimbaji wadogo nchini.
Waziri
 wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo (katikati waliokaa) 
akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita 
(GGM), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na  Wakuu wa 
Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa 
Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)
 na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao 
kilichofanyika mjini Geita. Wa Pili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Geita, 
Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga.
Na Teresia Mhagama, Geita.
MGODI 
wa Dhahabu wa Geita (GGM) uliopo mkoani Geita umeridhia ombi la Serikali
 la kutoa mabaki ya mawe ya  dhahabu kwa wananchi ili kuweza kuyachenjua
 na kupata dhahabu.
Hayo 
yameelezwa mjini Geita na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter 
Muhongo mara baada ya kumaliza vikao vya majadiliano kati ya watendaji 
wa GGM, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa 
Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa 
Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)
 na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
“Tatizo
 la Magwangala sasa limetatuliwa kwani Mgodi umekubali kuyatoa kwa 
wananchi ila kinachotakiwa kufanywa kabla ya kuyatoa magwangala hayo ni 
Serikali ya Mkoa huu kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kuhakikisha 
kuwa kwanza wanapata eneo ambalo uchenjuaji wa magwangala utafanyika,” 
alisema Profesa Muhongo.
Aidha 
aliongeza kuwa eneo hilo litakalotengwa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa 
Geita lazima lifanyiwe tathmini ya mazingira na Baraza la Hifadhi na 
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuweza kuthibitika kama eneo hilo 
linafaa kwa shughuli hizo bila kuleta athari kwa wananchi na mazingira.
Profesa
 Muhongo alitoa agizo kuwa  kazi hizo zinatakiwa kukamilika tarehe 30 
Juni, mwaka huu ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itafanya kikao 
kitakachohudhuriwa na watendaji wa  Mgodi na Wabunge wa mkoa huo na 
kutoa uthibitisho wa kimaandishi kuhusu eneo lililotengwa kwa shughuli 
hiyo pamoja na Cheti kutoka NEMC cha uthibitisho kuwa eneo hilo linafaa 
au halifai kwa shughuli za uchenjuaji madini kufanyika.
Aidha 
alieleza kuwa katika kikao hicho cha tarehe 30 Juni GGM itapaswa pia 
kutoa uthibitisho wa kimaandishi kuwa imekubali kutoa magwangala hayo 
kwa wananchi.
“Baada
 ya Eneo hilo na Cheti cha mazingira kupatikana,  sasa katika kikao 
hicho mtaweza kujadiliana kuhusu  usafirishaji wa magwangala  hayo 
kutoka eneo la Mgodi hadi eneo lililotengwa, hapo mtakubaliana nani 
atachukua jukumu la kusafirisha magwangala hayo,”alisema Profesa 
Muhongo.
Aliongeza
 kuwa Leseni za uchenjuaji madini zitakazotolewa mara baada ya eneo 
 hilo kupatikana, zitakuwa katika vikundi na si mtu mmoja mmoja  ambapo 
 Ofisi ya Mkuu wa mkoa ndiyo itakayoratibu suala hilo huku jukumu la 
Wizara likiwa ni kutoa Leseni hizo.
“Ni 
vizuri pia mkashirikiana na viongozi wa Wachimbaji Wadogo katika 
kuratibu uundaji wa vikundi hivyo na lazima vikundi hivyo vielezwe kuwa 
ni lazima walipe kodi stahiki kwa Serikali kama ilivyo kwa shughuli 
nyingine za uchenjuaji madini,” alisema Profesa Muhongo.
Kwa 
nyakati tofauti Wabunge wa mkoa huo walieleza kuwa utoaji wa Magwangala 
hayo kwa wananchi, utasaidia wanachi hao kujiajiri, kujiongezea kipato 
na kuwaepusha katika kushiriki matendo ya uhalifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni