Mbunge
wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai
katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge
la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.
...................................................................................................................
SERIKALI
ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria
kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015
wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga
uchumi wa Viwanda.
Wakati Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata
sapoti kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga
mkono hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika
eneo hilo.
Abdallah Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya
ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi
wake ameonesha dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa
kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.
Anasema kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana
ya wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono
miwili mageuzi haya kwani wameahidi hivyo lazima watende.
Ulega anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na linarutuba
ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza
viwanda vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali
Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
Anasema kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za
kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika
na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda.
"Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda."anasema ulega
Anasema kuwa kutokana na utajili wa Ardhi yenye rutuba wanaweza
kujenga viwanda vya kusindika mazao lakini pia kwa sababu eneo lao ni
kubwa basi hata viwanda vya kubangua korosho na kujengwa Kwa viwanda
hivyo kutasaidia kuleta ajira katika eneo hilo.
Anasisitiza kuwa ndio maana wakati akichangia mpango wa wa
maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano ameomba Serikali na wahisani
kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa Serikali kuiweka Mkuranga kuwa
sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda.
Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo lake la
kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna ajira
inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.
"Nimesema wazi kuwa Mkuranga kuna matatizo ya miundombinu
mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na mambo mengine na katika
baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya marafiki wameitikia mwito
wangu na wameweza kusaidia katika kichimba visima ambapo wananchi wangu
wameaza kupata Maji safi na salama."anasema Ulega
Anasema kuwa anawashukuru African Foundation Reflection Kwa
kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi hizo zote zimetokana na jitihada
zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga inakuwa ya kutolea mfano tofauti
na ilivyo sasa.
Aidha katika mpango huo wa maendeleo Kwa miaka mitano Kwa
Serikali ameomba kujengewa barabara Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa
kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni muhimu Kwa wananchi wa wilaya
hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.
Pia anasema katika mpango mpango wa pili wa maendeleo wa miaka
mitano Kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya
ya Mafia kwa sababu pale kuna bandari na watu wake pia ndiyo
wazalishaji wakubwa wa korosho na samaki.
Anasema kuwa pia kwenye kata yake ya mbezi kwaniaba ya
wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri Serikali kuwa eneo la viwanda
ili wananchi wake wawe sehemu ya uzalishaji wake.
Aidha Ulega anazungumzia suala la kuondoa kero ya uhaba wa
upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo Serikali ingefanya bidii ya
kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji kupitia kibiti hadi kufika
Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.
Anasema haiwezekani Kwa miaka nenda rudi tatizo la Maji
halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa kwa karibu na Mto Rufiji
ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji ikifanyika tatizo hilo litabaki
kuwa historia katika eneo hilo.
Anasema tatizo la ajira Kwa vijana ni kubwa mno hivyo
wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa kutilia mkazo uazishwaji na
ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo linaweza kuwa.msaada Kwa
vijana kuweza kupata ajira.
"Mimi kama Mbunge wao kama nilivyosema awali nitaendelea
kupambana na kufanya kila linalowezekana Kwa kuhakikisha Mkuranga
inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa rai Kwa wawekezaji
kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili vijana wangu
wapate ajira."anasema
Anaongeza kuwa mkuranga ilisahaulika mno pamoja kwamba ni
miongoni mwa wilaya za siku nyingi lakini imekuwa nyuma kimaendeleo
hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya
maendeleo.
Anasema kuwa wananchi wake waendelee kumuombea Kwa Mungu na
wazidi kudumisha Umoja na mshikamano ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo
la kuona jimbo la mkuranga linakuwa la mfano.
Akizungumzia kilimo cha korosho anasema kuwa pamoja na zao hilo
kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha maisha ya wananchi wake lakini
bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa viwanda hususani vya ubanguaji
kunafanya pasiwepo na tija sana wanayoipata wananchi wake katika kilimo
hicho.
Anasema kuwa kutokana na hali hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea
kuzungumza na watu mbalimbali ili kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza
kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
Pia akizungumzia Elimu anasema anatambua changamoto zilizopo
katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa dhati Kwa kushirikiana na
Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi ili waweze kufanya vema
katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata wataalamu wa baadae.
"Najua kuna Changamoto ya madawati na hili tunalishugulikia Kwa
kushirikiana na kamati mbalimbali za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili
kuona namna ya kukabiliana na tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo
."anasema Ulega.
Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja
kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais
Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni