
Akinamama
 wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na 
mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi
 wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada
 ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.

Mama
 Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of 
Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices 
wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.

Akinamama
 wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na 
mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi 
wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya 
kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.
Ziara ya mafunzo kujifunza jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.
Ziara ya mafunzo kujifunza majiko yanayotumia nishati ya jua.
Ziara ya mafunzo katika chumba cha habari cha gazeti la El Pais.
Akimama na wawezeshaji wa mafunzo katika picha ya pamoja darasani.
WANAWAKE
 wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa 
jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na 
mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya 
wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa  inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama  María Teresa Fernández de laVega.
Taasisi
 hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi 
inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao 
ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza 
mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za 
akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una
 lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na 
mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza 
zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya 
tabianchi.
Mradi
 huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira 
(EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika 
mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na 
Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.
Mratibu
 wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi 
ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za 
mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti
 ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe 
mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa 
mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro. 
Miradi
 mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani 
Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es 
Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko 
linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.
Mradi
 huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama 
kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao 
kusikika. Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira
 kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa 
familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi 
mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa
 Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu 
cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa 
habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain 
inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku 
nchini zinaweza kutumika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo 
kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na 
jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya 
tabianchi.
Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.  




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni