Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya
Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa
Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni
mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe
huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la
Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la
Afrika Mhe. Bennette hayatoe
Wabunge
wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu.
Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile,
Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.
Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika
liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina
budi kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe. Ndugai
aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge
hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia
changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi
barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya
wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji
suluhisho la Pamoja kuyakabili..
“ katika duniani ya sasa ni
vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri
hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea
eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa
wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani”
alisema Ndugai
Akizungumzia nafasi ya wabunge katika kupiga
vita changamoto zinazolikabili bara la Afrika, Mhe. Ndugai amesema
wabunge wa Bunge la Afrika kama wawakilishi wa Manbunge ya Nchi
wanachama wa Umoja wa Afrika wanawajibu wa kutetea maslahi ya Bara la
Afrika bila kujali itikadi za kisiasa, maeneo wanayotoka na mambo
mengine yanayoweza kuligawa bara la Afrika.
“ Mkiwa Wabunge
mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima mhakikishe Umoja wa
Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la Afrika ili kutimiza ndoto
waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika. Kwa mfano baba wa Taifa
la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alisema lazima tukimbie
wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai
Mapema akitoa
salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Mhe. Nthloi
Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na waasisi
wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na kuwataka
wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa ya
kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.
Katika hatua
nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la
Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge hilo baada ya
Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.
Wabunge hao
ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni Mhita, Mhe. David
Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai anatarajia kurejea nchini
kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika linaendelea na Vikao vyake hadi
tarehe 13 Mei, 2016.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni