Uongozi wa Kampuni ya Tanzanite
One ya wilayani Simanjiro Mkoani Manyara umesema kuwa Mbunge wa jimbo la
Simanjiro ,James Ole Millya amelipotosha bunge na umma kwa ujumla kwa
kusema kauli ambazo hakuzifanyia utafiti wa kina.
Millya katika kikao cha Juzi
bungeni alisema kuwa kampuni ya Sky Group Associates iliyonunua hisa kwa
kampuni ya Tanzanite One na kumiliki kitalu C cha madini ya Tanzanite
Mererani wilayani humo hakikufuata taratibu za ununuaji wa hisa hizo na
kuwatuhumu baadhi ya Mawaziri kuwa walihusika katika kupindisha
taratibu.
Mbali ya hilo Mbunge huyo alienda
mbali zaidi na kuituhumu kampuni hiyo kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi
201 bila ya kufuata utaratibu na kuwa kampuni ya Tanzanite One
inanyanyasa wafanyakazi.
Akizungumza kwa njia ya simu
mwanasheria wa kampuni hiyo,Kisaka Mzava alisema uongozi wa Tanmzanite
One umesikitishwa na kauli ya Mbunge Millya aliyesomea taaluma ya sheria
kwa kusema vitu ambavyo hafanyia utafiti wa kina hatua ambayo uongozi
unashaka na taaluma yake kwani vitu kama hivyo hata mtoto mdogo hawezi
kusema.
Mzava alisema na kumtaka mbunge
huyo kwanza kujilidhisha kwa kufanya utafiti wa kina namna hisa za
Tanzanite One zilizouzwa kwa kampuni ya Sky Group inayomilikiwa na
wazawa kwa asilimia mia na wamiliki wa hisa wanajulikana na kama
anahitaji kujuwa anapaswa kwenda Brella kujilidhisha.
Alisema hakuna Waziri wala
kiongozi yoyote mwingine wa serikali anayemiliki hisa katika kampuni
hiyo na kulichosemwa na Mbunge Millya kinapaswa kulaaniwa.
Mwansheria huyo alisema Sky Group
katika ununuzi wa hisa hizo umeshalipa kodi ya serikali yote bila ya
wasiwasi na kampuni hiyo sio kampuni ya mfukoni kama anavyodai kwani
mbunge huyo amelipotosha bunge na umma kwa ujumla kwa maslahi yake
binafsi.
Mwanasheria huyo alisema shughuli
za uzalishaji zinasimamiwa kikamilifu kati ya kampuni ya Sky Group na
serikali kupitia Stamico na hakuna madini yanayoibiwa kama Mbunge huyo
anavyosema na kama ana ushahidi wa wizi huo anapaswa kuutoa nje ya
bunge.
Alisema hakuna njia ya mkato
iliyofanywa katika ununuwaji wa hisa na hakuna Waziri yoyote aliyehusika
katika kusaidia kupindisha taratibu kwani kila kitu kipo wazi na
alichosema mbunge Millya anapaswa kukitolea ushahidi nje ya bunge na sio
ndani ya bunge.
Akizungumzia kufukuzwa kwa
wafanyakazi,mwanasheria huyo alisema kuwa wafanyakazi 201 waliofukuzwa
kazi ni wafanyakazi hatari kwa mstakabali wa kampuni kwani ni
wachochezi,na wenye hila za kutaka kuihujumu kampuni hiyo ili iweze
kuleta maafa.
Mwanasheria huyo alisema kugoma
ni kosa kisheria kama mgomo hakufuata taratibu sheria lazima zichukue
taratibu na ndio uongozi wa Tanzanite One umechukua kwa kuwafukuza kazi
wafanyakazi hao 201 walipogoma bila ya kufuata taratibu.
‘’Sheria za kazi ziko wazi
kugoma,kuhujumu kampuni na kuchochea wafanyakazi kugoma na kuhujumu
kampuni ni kosa kisheria hivyo uongozi wa kampuni haukusita kuwachukulia
hatua kwa hilo’’
‘’Wafanyakazi waliofukuzwa kazi
walistahili kufukuzwa na kama kampuni ilikiuka taratibu sheria iko na
vyombo vya kisheria viko na siasa isiingizwe katika masuala ya
kisheria’’
Mwanasheria huyo alisema Waziri
wa Nchi,ofisi ya Waziri Mkuu sera,Bunge,kazi ajira vijana na walemavu
Jenista Mhagama hana ndugu na mtu anayefanya kazi katika kampuni ya
Tanzanite One na kilichosemwa na Mbunge Millya ni kukurupuka na uongo wa
kupindukia ambao haukufanyiwa utafiti wa kina.
Mzava alisema Nasibu Mhagama ana
mtoto anaitwa Yufuph Mhagama ambaye anafanya kazi Tanzanite One na
hawana uhusiano wowote na Waziri Mhagama na wala hawamujii.
‘’ Yusuph Mhagama ni mtoto wa
Nasibu Mhagama hawana uhusiano wowte na waziri Jenista Mhagama na wala
hawamjui’’ Mwanasheria huyo
Kampuni imesikitishwa sana na
upotoshwaji ulitolewa ndani ya bunge na mbunge Millya na inashaka na
taaluma ya sheria ya mbunge huyo kwani hakufanyia utafiti hoja
aliziwasilisha bungeni na kuonekana kutumika kwa maslahi yao watu
wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni