MKUU WA WILAYA YA IRINGA, MH. KASESELA ATOA RAI KWA MANISPAA YA IRINGA KUONGEZA KASI YA KUKUSANYA MAPATO

Mstahiki meya Mh Alex Kimbe akifungua baraza
Mh Leah Leah Mleleu Diwani viti Maalum (CHADEMA) akisiliza kwa makini
Mh Peter Msigwa akichangia hoja
Mh Richard Kasesela akitoa hotuba yake kwa baraza hilo
Mh Dadi Igogo Diwani wa Gangilonga akiwasilisha hoja binafsi inayo husu vikao vya baraza kurushwa live moja kwa moja ili wananchi wote wa Iringa wafuatilie.

Mh Nyalusi akichangia hoja 

Mkuu wa wilaya Iringa akiudhuria kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Iringa na kutoa rai kuhakikisha waheshimiwa madiwani wana buni mbinu mpya za kukusanya mapato zisizo waumiza wananchi, mfano gereji ya manispaa ingeweza kutumika kukagua magari kwa kushirkiana na polisi. 

Katika hotuba yake alisisitiza suala la Ulinzi na usalama hasa ulinzi wa Mtoto na mama, kwani sasa imekuwa kawaida wanaume kupiga wake zao na kukosa utu. 

Pia watoto wana bakwa lakini taarifa hazifiki kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, zile zinazo fika ziapungikiwa ushahidi. Mheshimiwa Kasesela amesitiza suala mipango miji endelevu yenye kufikiria mbali zaidi, nyumba zote ambazo hazifai kwa makazi wahusika waambiwe. 

Vichoro vyote vilivyo fungwa vifunguliwa ili kuondoa hali hatarishi. Kwa upande wa elimu alitoa Msistizo mkubwa kwa kila diwani ulikuwa kuhakikisha kila shule inakuwa na madawati ya kutosha. 

Baraza hilo lilifunguliwa na Mstahiki meya Mh. Alex Kimbe, pia alikuwapo Naibu meya Bwana Nzala Lyata, Mbunge wa Iringa mjini mh Peter Msigwa. Madwani walijadili mapendekezo ya vikao vya kamti mbalimbali na kupitisha maazimio yote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni