Afisa polisi mmoja ameuwawa kwa
mlipuko uliokuwa ndani ya gari karibu na Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi kusini mashariki mwa mji wa Gaziantep nchini Uturuki.
Maafisa polisi 19 na raia wanne
wameripotiwa kujeruhiwa na mlipuko huo uliotokea leo asubuhi.
Uturuki imekuwa ikikumbwa na matukio
ya mfululizo ya milipuko tangu mwaka uliopita, inayofanywa na
wapiganaji wa Kikurdi na Dola ya Kiislam (IS).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni