Kudorora kwa uchumi wa Venezuela
kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, kumeiathiri sekta ya afya
ambapo hospitali sasa hazina umeme, dawa, vitanda na hata sabuni
ambapo hali ni mbaya mno.
Hospitali za Venezuela pia
zinamazingira machafu, wagonjwa wenye kutokwa damu wakiwa
wametelekezwa na damu zao kuchuruzika kwenye sakafu za hospitali,
madaktari nao wanalazimika kufanya upasuaji bila vifaa.
Hali hiyo imebainika huku rais wa
Venezuela, Nicolas Maduro, akidai kuwa nchi yake hiyo inahuduma bora
za tiba duniani ikiwa nyuma baada ya taifa la Cuba, jambo ambalo ni
tofauti na uhalisia.
Wagonjwa waliovunjika miguu wakipatiwa matibabu kwa kutumia madumu ya maji badala ya vyuma vizito
Mama akiwa na mtoto wake mwenye tatizo la pumu akimpatia msaada wa kumshikilia kifaa cha oxygen
Mgonjwa aliyeumia vibaya sehemu ya kichwa akiwa hospitali akingojea kwa mwaka mzima kufanyiwa upasuaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni