mbunge wa bunge la Afrika mashariki Shyrose Bhanji akiongea katika bunge hilo jijini Arusha jana kuelezea wigo mapana unatakiwa ili serikali isipoteze kodi 
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
 Serekali imekuwa
inapoteza kodi nyingi  zinazotokana  na ushuru wa mazoao kutokana na kuwa na
mzabuni  mmoja ambaye anakusanya  kodi za mazao 
kwa nchi nzima .
Hayo yamebainishwa na  mbunge wa  EALA, Shy-Rose 
Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge
hilo   ambapo alisema kuwa kuna changamoto
kubwa  ya utekelezaji wa umoja wa forodha
hapa nchini Tanzania.
Alisema kuwa  wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao
wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali 
zinazofikia kiwango   staili cha
asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa awatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao
katika  nchi za jumuiya wanachama .
 Aidha alibainisha
kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande  wa
Tanzania kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi  au kubaini viwango vya kusamehewa kodi
zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya tccia.
Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa  upya katika nchi yetu na serekali kwasababu
TCCIA aipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni
mikoa tu  huku katika ngazi za wilaya
pamoja na vijiji awapatikani.
Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na
pia wananchi wengi  pamoja na wafanya
biashara wengi kutokujua dhamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha
mfanyabiashara kujua unafuu wa wa kodi.
“sasa ivi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na
wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa 
dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa jukumu la kutoa
hati  hizi kwa wadau wengine ili kuleta
unafuu wakodi “alisema Bhanji
Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za
biashara za manispaa pamoja na  ofisi za
biashara za  wialaya nawao waweze
kupewa  ili jukumu na wao waweze kutoa
hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji
na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni