Watoto mapacha walioungana mwili
waliozaliwa hospitali ya rufaa ya Pwani mjini Mombasa nchini Kenya
wamefariki dunia leo alfajiri.
Watoto hao walizaliwa Alhamisi na
walikuwa wasafirishwe kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa ya Kenyatta
kwa matibabu maalum wamefariki wakiwa kwenye chumba cha wagonjwa
mahututi.
Akithibitisha vifo vya mapacha hao
Mtendaji Mkuu CPGH Dk. Iqbal Khandwalla ameviambia vyombo vya habari
vya Kenya kwamba jitihada za madaktari za kuokoa maisha ya watoto hao
zimeshindikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni