Mwanaume
aliyevua nguo zote na kisha kujirushwa kwenye chumba cha simba
nchini Chile kwa lengo la kujiuwa amenusurika kifo, lakini ni baada
ya simba hao kuuwawa.
Mamlaka za Jiji
la Santiago zimethibitisha kutokea kwa tuko hilo ambapo simba wawili
waliuwawa wakati wakimg'ata mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 20
siku ya jana.
Mwanaume huyo
aliyetambulika kwa jina la Franco Luiss Ferrada Roman alikimbizwa
hospitali iliyopo karibu kwa matibabu na hali yaki inasemekana ni
mbaya.
                     Simba wakimg'ata mtu huyo aliyetumbukiwa kwenye chumba chao
Mwanaume
 aliyejitumbukiza kwenye chumba cha simba akiwa amemkumbatia kwa mikono 
na miguu simba dume aliyekuwa akimng'ata shingoni



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni