Benki ya 
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yatoa mkopo wa 890 Milioni kwa 
wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji 
katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilombero ili kuongeza tija na 
uzalishaji wa zao la mpunga.
Hayo 
yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert
 Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa 
morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya 
ya Kilombero.
Bw. 
Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350 
ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa 
utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na 
kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu 
kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
 umaskini.
“Mkopo 
huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika 
kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha 
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika
 kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.
Kwa 
mujibu wa Bw. Paschal mkopo huo utasaidia shughuli mbalimbali za 
utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho 
vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mpunga pamoja na kuwezesha 
upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa.
Mkurugenzi
 huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye 
ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa 
mitambo ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.
“Tunaamini
 mkopo huu utachagiza kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la 
Taifa kutokana kuongezeka kwa tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya 
ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo hivyo 
kuchangia kuongezeka kwa ajira nchini,” aliongeza. 
Akizungumzia
 mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa 
mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa
 kutumia njia mbalimbali. Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo 
mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo;
 kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa 
mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na 
mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa 
fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.
“Kwa 
kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya 
uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo 
cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji 
kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi 
kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye 
kuendeleza kilimo,” alisema.
Warsha 
hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe 
ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha
 hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na 
TADB. Mhe. Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na 
Benki hii na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali
“Nawasihi
 mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze 
kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma 
kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni