BENKI
ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wamewapa semina
wateja wajasiliamali wa benki hiyo kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya
Mtandao yaani Internet Banking.
Huduma ya Internet
Banking itawajengea uwezo wajasiliamali hao katika nyanja mbalimbali
kama vile kuwalipa mshahara wafanyakazi wake, kuangalia jumala ya mapata
waliyanayo kwenye akaunti yake pamoja na kuangali jinsi pesa
ilivyowekwa na kutolewa katika akaunti yako kwa njia ya mtandao wa
Interneti.
Mkurugenzi
wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango akizungumza
katika semina ya wajasiliamali wenye akaunti za benki ya CRDB jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
wa huduma mbadala za benki ya CRDB jijini Dar es Salaam, Dr. Joseph
Witts akizungumza na wajasiliamali wenye akaunti kwenye benki ya CRDB
katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo tawi la Mlimani City jijini
Dar es Salaam.
Meneja
huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ya kieletroniki, Mangire Kibanda
akifafanua juu ya huduma ya Interneti banking kwa wajasiliamali wenye
akaunti za benki ya CRDB jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano
wa Ubungo plaza.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es
Salaam wakiwa katika semina ya wajasiliamali wenye akaunti za Benki za
CRDB.
Baadhi
wajasiliamali wakimsikiliza Meneja huduma za kibenki kwa njia ya
mtandao ya kieletroniki, Mangire Kibanda katika semina iliyoandaliwa na
wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni