Meneja Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. James Mlowe amekabidhi Jumla ya madawati 124 kwa
ajili ya shule za Manispaa ya Kinondoni, msaada huo umetolewa na
taasisi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 10,000,000/=
yamekabidhiwa kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ali
Hapi. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa
madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya
Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa
Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Salum Ally Hapi (kulia) akipokea msaada wa madawati 124 kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa
mfuko wa pensheni wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya shule za Serikali
Manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Katikati ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum Ally Hapi akizungumza
katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni
wa LAPF jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni