SERIKALI ITAENDELEA KUTHAMINI NA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MICHEZO YOTE

B1 
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally Mzunguko wa Pili jana jijini Dar es Salaam. Ambapo zaidi ya magari 15 yanashiriki katika viwanja vya vilivyopo wilayani Bagamoyo.
B2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisikililiza kwa makini maelezo kuhusu mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally kutoka kwa Mratibu wa mashindano hayo ambaye pi ni Mwenyekiti wa Mzizima Motors Sports Club Bi. Hidaya Kamaga (katikati) jana jijini Dar es Salaam. Aliyesimamani ni mshiriki wa mashindano hayo kutoka Timu ya Puma Energy Bw. Dharam Pandya.
B3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiangalia moja ya magari yanayotumika katika mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally jana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge.
B4
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiruhusu gari ambalo linawakilisha timu ya wasanii wa Bongo Movie kuanza safari ya kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani tayari kwa mashindano ya Alliance Auto MMSC Rally jana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge na Katibu wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.Timu hiyo ya Bongo movie imeshiriki katika mbio hizo kwa lengo la kuhamasisha uanzishwaji wa Mfuko wa Filamu Tanzania.
B9
Mmoja wa washiriki wa mbashindano ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally kutoka Timu ya Hari Singh ya Moshi Kilimanjaro Bw.Gujrit Dhani akielezea jambo mara baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mashindano hayo jana wilayani Bagamoyo.
B5
B6 B7
Baadhi ya magari yakiwa katika mashindano ya Alliance Auto MMSC Rally yanayofikia tamati leo mjini Bagamoyo.
B8
Baadhi ya mashabiki wa mchezo wa mbio za magari wakifuatilia mbio za Alliance Auto MMSC Rally mzungoko wa Pili jana wilayani Bagamoyo.B10
Baadhi ya watazamaji wa mbio za magari wakirejea makwao mara baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally jana wilayani Bagamoyo. Picha na Frank Shija, WHUSM.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni