SHAKA AITAKA MIKOA YA KASKAZINI KUKATAA SIASA ZA UKANDA NA UZAWA


Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa  SHAKA HAMDU SHAKA akabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga

 Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anafungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a
kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa  kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwa wasili wilayani Mwanga

katibu wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Yasin Lema  akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya UVCCM wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro


Na Woinde Shizza, Mwanga

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.

Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka  katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba   kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au  damu imwagike.

Hayo yamelezwa leo   na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kata ya Mwanga mkoani hapa.

Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa anaishi, kupigania madaraka., vyeo au utawala kwa kutumia maneno au sera za  ubaguzi wa dini, ukabila, uzawa au ukanda.

Aidha aliongeza kuwa  baada ya miaka 52 ya uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika na zanzibar, anapotokea kiiobgozi au chama cha siasa kinachokifanya shughuli za kisiasa kwa kueneza sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa ukanda ni hatari mpya mbele ya watanzania.

"Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna hatari inawanyemelea, msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka kwake ni mbinde, ili ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo  si ajabu damu ikanwagika "alisema Shaka

Alisema wakati baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo wakiaza kughilibiwa na wanasiasa uchwara wakubali kuchagua vyana kwa sababu za ukanda na ukabila, idadi kubwa ya wakaazi wa Mikao hiyo wanaishi na wamejijenga kiuchumi  katika mikoa mingine ya nchi na huko hawabughudhiwi wala kubaguliwa.

"Haiikisha mkiendela kubagua wenzetu  na nyinyi mtaanza kubaguliwa,vdhambi ya ubaguzi haina toba, kataeni siasa chafu na wakwepeni matapeli wa kisiasa na walafi wa madaraka  "alisisitiza shaka.

Kaimu huyo katibu mkuu wa UVCCM alisema kwamba Taifa la Tanania halikuachwa na wakoloni bali liliundwa na waasisi wake Marehemu baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume bila na kupiga vita ubaguzi wa  kikabila, udini, rangi za watu au kuendekeza uzawa.

Alisema kutendo chochote kitakachopelekea  kuacha au  kuipuuza  misingi ya Taifa letu ambayo  imewafanya watu kuwa na umoja, upendo na mshikamano   radhi za waasisi hao pamoja na za  wenzao zitaigeukia nchi yetu iwapo  tutakubali kugawanywa na wanasiasa wachovu.

Kwa upande  wake Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma alisisitiza haja ya kuendelea kuheshimu na kudumisha umoja wa kitaifa nchini na mwanasiasa yeyote atakayeonekaa kana ni mkabila, mdini na asiyehimiza amani na utulivu aogopwe kama ebola.

"Ni mkoa upi leo hii nchini kwetu ambao wanaishi janii ya watu wa kabila moja,dini moja,rangi moja au ukoo mmoja,tikate ukabila ns vyama vilivyoanza kuonyesha ubaguzi wa aina yeyote "alisema Raibu

Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoani kilimanjaro alisema vyama vinavyopita na kueneza siasa za chuki, ukanda au ukabila vichunguzwe na ikiwa vitatjibiiyika kujihusisha na vitendo hivyo hatari  Msajili wa Vyama vya siasa nchini  achukue hatua za kisheria kuifuta mara moja kabla havijaleta madhara.

Shaka na msafara wake wanaendelea na ziara katika wilaya ya Mwanga kabla ya kuhitimisha wilaya ya Same baadae kuelekea
Mkoani Tanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni