Muandaaji
 wa tamasha la michezo kwa vijana wa mkoa wa Arusha Neema Mollel ambaye 
pia ni  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina pamoja na  mlezi wa Timu za 
mpira kata ya Sakina Jijini Arusha akiongea katika fainali za Tamasha la
 vijana lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
 jijini hapa.
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Olmatejoo A.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Diwani wa kata ya Ungalimited akiwa anawaasa vijana kuachana na madawa ya kulevya katika fainali hizo
Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.
 …………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Timu
 ya Intersport Club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana  mara baada
 ya  kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika 
katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.
 Tamsha
 hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia 
tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo 
kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi 
kikubwa  
Akizungumza
 wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo 
ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa 
lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na 
kuwapa elimu  ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa 
vijana 
Alisema
 kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya 
kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa
 elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo 
limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua 
kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua 
kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo
 “nia
 alisi ya  kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja 
na kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana 
pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani 
michezo ni ajira”Alisema Neema Mollel
Aidha
 aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara 
ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia 
lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na
jamii.
jamii.
Akikabidhi
 kombe kwa washindi ambao ni Interspot Club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya
 Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati
 ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya 
kijana ufahamu wake kuchangamka.
Sambamba
 ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club
 kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na  Tsh 100,000 
,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black 
Eagle Tsh 50,000. 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni