MADAKTARI BINGWA WA MACHO KUTOKA JUMUIYA YA LOUIS NIELSEN YA DENMARK WAWAFANYIA UCHUNGUZI WA MACHO WANANCHI NA KUTOA MIWANI BILA YA MALIPO

Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo akizungumza na madaktari bingwa wa macho kutoka Jumuia ya Louis Nielsen ya Denmark ambao wapo Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma ya miwani kwa wananchi katika Skuli ya Msingi Kiembesamaki Mjini Zanzibar.
Daktari Pernille Overgaard kutoka Debmark akimfanyia uchunguzi wa macho Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Skuli ya msingi ya Kiembesamaki.
Wananachi waliofika Skuli ya msingi ya Kiembesamaki kufanyiwa uchunguzi wa macho wakiwa kwenye mistari kusubiri zamu zao kuonana na madaktari bingwa wa macho kutoka Denmark.
Baadhi ya wananchi waliofanyiwa uchunguzi wa macho na madaktari kutoka Denmark wakisubiri kupatiwa msaada wa miwani za bure kutoka kwa madaktari hao. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

WATUMISHI WAWILI WA SERIKALINI WAFUKUZWA KAZI NA DED WA ILEJE

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi akiongea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Wilaya ya Ileje.

                                                                                                 Na fredy mgunda,Ileje

BARAZA la Madiwani Wilayani Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili wa Halmashauri hiyo kutokanana makosa ya wizi wa mamillioni ya fedha za wafadhili za mradi wa UKIMWI wa water reed
 

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la pili Josephat Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya zaidi Milioni 84.

“Josephati aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200 /-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha shilingi milioni 48742500/-fedha za mradi wa Water Aid zilizofika katika Halmashauri ya wilaya ya Ileje”alisema Songa

Mwenyekiti huyo ameagiza watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha katika Akaunti ya Halmashauri hili ziweze kufanya kazi zingine.

kwa mtumishi mwengine Anna mwakipesile kesi yake bado inaendelea na uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na ras songwe waliachiwa huru na kurudishwa kazini baada ya tume kuridhika na utetezi wao

Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa shule wawili ambao ni Henry Musomba wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu na matumizi mabaya ralislimali

Aidha Mnasi alisema kuwa ni wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini kujitathimni kwa kile alichofanya kwani waliotuhumiwa ni wengi lakini bado uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo kwani kila mmoja atakayebainika kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.

Ametoa onyo kwa watumishi kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wa kwa kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali aitamfumbiamcaho kwani hu ni wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa maslahii ya Taifa.

“Mimi sipo tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli” alisema Mnasi

JAMBAZI MMOJA AUAWA KWA RISASI AKIPORA ABIRIA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya jambazi hilo lililowawa

                                            Na Mahmoud Ahmad,Arusha

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Monduli kwa ajili ya matibabu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alipoongea na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea muda saa 07:00 Usiku maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.

Kamanda Mkumbo alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na bunduki ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na marungu ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo likitokea Moshi kuelekea mkoani Singida.

‘’Mara baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa Majengo Moshi ambapo walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung pamoja na fedha taslimu Tsh 50,000/=’’.

“Wakati wanaendelea na tukio hilo askari Polisi waliokuwa High Way Patrol walipata taarifa za tukio hilo ambapo walikwenda kwa haraka na mara baada ya majambazi hao kuwaona walianza kufyatua risasi hovyo na Polisi kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmojawao na kuwakamata wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne huku wengine akiwemo na yule mwenye bunduki wakikimbia”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa haraka, huku akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila kuvuja jasho kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.

UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE

Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .

Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .

Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.

Mwasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha na Mahmoud Ahmad Arusha).

Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.

Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia) walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea jijini Arusha.
Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.

KIOTA KIPYA ,BENDI MPYA YA MJENGONI VYWAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA MAMIA WAJITOKEZA KWEYE UZINDUZI HUO

Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
  Wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni kabu pamoja na mjengoni band wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza)
 Bendi mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
 mashabiki na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii


Msaniii wa bendi ya Fm Academia Kingombe Blaise na aliuthuria katika uzinduzi huu wa bandi ya mjengoni pamoja na klabu mpya matata ya Mjengon
Mmiliki wa blog ya libenee la kaskazini Woinde Shizza wa kwanza kulia nyuma yake ni mmiliki wa blog ya Jamii blog Pamela mollel ,wakanza kushoto ni dada Fatuma wa Stax Tv pamoja na Veronica Ignatus wote tulibahatika kuhuthuria na kushuhudia uzinduzi rasmi wa bendi ya mjengoni pamoja na klabu ya mjengoni
 Jiji la Arusha kwa nyama ni penyewe na pia klabu ya mjengoni kwa kuchoma nyama nzuri ndio pamonaongoza wadau wengi walionekana kuvutiwa na nyama ilikuwa imechoma na wataaalam wa klabu hiyo
Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliouthuria uzinduzi huo
 Burudani ikiendelea kutoka kwa bendi ya mjengoni








mmiliki wa jamii blog Pamela mollel akiwa anafafanua jambo kuhusiana na kiota iki kipya kilichozinduliwa rasmi jijini Arusha ambapo alitumia muda huo kuwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na wale wageni ambao wanauthuria katika mkoa huu kutoacha kufika mjengoni klabu kwa ajili ya kujipatia nyama choma safi na freshi pamoja na muziki muzuri kutoka katiak bendi ya mjengoni

habari picha na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog 
Bendi mpya  ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Bandi  imezinduliwa rasmi mkoani Arusha  huku ikiwaaidi mema wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia ndani ya jiji hilo

Akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi rasmi wa bendi hiyo Rais wa bendi  Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM Academia na malaika bendi.

Alisema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa wakitegemea bendi kutoka jijini dar lakini kwa sasa  ivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na itakuwa kila siku za wekendi

 Aidha alibaiisha kuwa bendi hiyo anayoisimania inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu  pamoja na uzoefu wakutosha ivyo anaamini wapenzi wa mziki wa dance wataipenda bendi hiyo na kuikubali

Alisema adi sasa bendi na inanyimbo zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze kupata mziki  na kuhusikia katika maredio na hata wanapokuwa majumbani

Alimalizia kwakusema kuwa bendi hiyo ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi  hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia wajitokeze kuja kupata burudani ya nguvu inayotoka kwa wanamuziki wa bendi hiyo.

Kwa upande wake wa mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme  alisema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa live bandi



Alisema kuwa kimepita kipindi kirefu wakazi wa jiji la Arusha wamekuwa wanakosa sehemu ya kwenda kupata burudani nzuri ya mziki wa bakurutu pamoja na live bendi inayoeleweka tangu hotel ya sabasaba ifungwe ivyo ameamua kuileta burudani hiyo ili wananchi wa Arusha waweze kupata sehemu ya kustarehe

Alimewakaribisha  wageni kutoka mikoani pindi wanapofika jijini Arusha kutoaacha kuja mjengoni kujipatia burudani ya nguvu kutoka katika bendi ya mjengoni pamoja na nyama choma nzuri na freshi inayotengenezwa na wachoma nyama waliobobea katika sekta hiyo.

 watu wakila bata
 huyu ndio mpiga kinanda



Rais wa Bendi ya Mjengoni akiimba kwa hisia

RAIS BARACK OBAMA NA MKEWE MICHELLE WAANDAA SHEREHE YA HALLOWEEN


Rais Barack Obama ameangusha bonge la sherehe ya Halloween katika Ikulu ya Marekani hapo jana, ambapo yeye na mkewe walicheza wimbo wa Thriller wa Michael Jackson.

Obama na Mkewe Michelle waligawa zawaidi mbalimbali kwa watoto wanajeshi, wa Marekani walioalikwa zikiwemo za pipi.
          Michelle Obama akifurahia jambo na mtoto aliyevalia nguo kama mtoto wa bata
                      Rais Obama na Mkewe Michelle wakigawa zawadi za tofi kwa watoto 
Michelle Obama akichangamsha sherehe hiyo huku mumewe rais Obama akimuangalia na kucheka

                                                        Sherehe hiyo ya Halloween iliendana na sarakasi

MANCHESTER UNITED YASAIDIA UNICEF KUKUSANYA PAUNDI LAKI MBILI


Jose Mourinho na wachezaji wake wa Manchester United waliamua kuweka kando hali yao ngumu katika ligi, na kuhudhuria mlo wa jioni ulioandaliwa na shirika la UNICEF na kusaidia kuchangishwa paundi 215,000 za msaada.

Mourinho pekee alisaidia kukusanywa paundi 30,000 kwa kuuza vitu vyake, saini yake, sweta la Adidas, nguo ya juu ya mazoezi pamoja na kitambaa cha skafu, na kisha kuamua kuitoa saa yake aliyovaa inayouzwa paundi 16,000.
       Kocha Jose Mourinho akivua saa yake aliyoitoa ipigwe mnada kuchangisha fedha 

                            Wachezaji wa Manchester United wakiwa katika picha ya pamoja