MANCHESTER UNITED YASAIDIA UNICEF KUKUSANYA PAUNDI LAKI MBILI


Jose Mourinho na wachezaji wake wa Manchester United waliamua kuweka kando hali yao ngumu katika ligi, na kuhudhuria mlo wa jioni ulioandaliwa na shirika la UNICEF na kusaidia kuchangishwa paundi 215,000 za msaada.

Mourinho pekee alisaidia kukusanywa paundi 30,000 kwa kuuza vitu vyake, saini yake, sweta la Adidas, nguo ya juu ya mazoezi pamoja na kitambaa cha skafu, na kisha kuamua kuitoa saa yake aliyovaa inayouzwa paundi 16,000.
       Kocha Jose Mourinho akivua saa yake aliyoitoa ipigwe mnada kuchangisha fedha 

                            Wachezaji wa Manchester United wakiwa katika picha ya pamoja

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni