Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
Wadau
waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni kabu pamoja na mjengoni band
wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza)
Bendi
mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni
waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
mashabiki na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii
Msaniii wa bendi ya Fm Academia Kingombe Blaise na aliuthuria katika uzinduzi huu wa bandi ya mjengoni pamoja na klabu mpya matata ya Mjengon
Mmiliki wa blog ya libenee la kaskazini Woinde Shizza wa kwanza kulia
nyuma yake ni mmiliki wa blog ya Jamii blog Pamela mollel ,wakanza
kushoto ni dada Fatuma wa Stax Tv pamoja na Veronica Ignatus wote
tulibahatika kuhuthuria na kushuhudia uzinduzi rasmi wa bendi ya
mjengoni pamoja na klabu ya mjengoni
Jiji
la Arusha kwa nyama ni penyewe na pia klabu ya mjengoni kwa kuchoma
nyama nzuri ndio pamonaongoza wadau wengi walionekana kuvutiwa na nyama
ilikuwa imechoma na wataaalam wa klabu hiyo
Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliouthuria uzinduzi huo
Burudani ikiendelea kutoka kwa bendi ya mjengoni
mmiliki wa jamii blog Pamela mollel akiwa anafafanua jambo kuhusiana na
kiota iki kipya kilichozinduliwa rasmi jijini Arusha ambapo alitumia
muda huo kuwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na wale wageni ambao
wanauthuria katika mkoa huu kutoacha kufika mjengoni klabu kwa ajili
ya kujipatia nyama choma safi na freshi pamoja na muziki muzuri kutoka
katiak bendi ya mjengoni
|
habari picha na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog
Bendi mpya ya mziki wa dance
ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Bandi imezinduliwa rasmi mkoani
Arusha huku ikiwaaidi mema wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni
wanaoingia ndani ya jiji hilo
Akiongea na waandishi wa habari
katika usiku wa uzinduzi rasmi wa bendi hiyo Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa
wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya
nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM
Academia na malaika bendi.
Alisema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa
wakitegemea bendi kutoka jijini dar lakini kwa sasa ivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na
itakuwa kila siku za wekendi
Aidha alibaiisha kuwa bendi hiyo anayoisimania
inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu pamoja na uzoefu wakutosha ivyo anaamini
wapenzi wa mziki wa dance wataipenda bendi hiyo na kuikubali
Alisema adi sasa bendi na inanyimbo
zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze
kupata mziki na kuhusikia katika maredio
na hata wanapokuwa majumbani
Alimalizia kwakusema kuwa bendi hiyo
ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na
wageni wanaoingia wajitokeze kuja kupata burudani ya nguvu inayotoka kwa
wanamuziki wa bendi hiyo.
Kwa upande wake wa mkurugenzi wa
mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme alisema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya
ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata
chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa live bandi
Alisema kuwa kimepita kipindi kirefu
wakazi wa jiji la Arusha wamekuwa wanakosa sehemu ya kwenda kupata burudani
nzuri ya mziki wa bakurutu pamoja na live bendi inayoeleweka tangu hotel ya
sabasaba ifungwe ivyo ameamua kuileta burudani hiyo ili wananchi wa Arusha
waweze kupata sehemu ya kustarehe
Alimewakaribisha wageni kutoka mikoani pindi wanapofika jijini
Arusha kutoaacha kuja mjengoni kujipatia burudani ya nguvu kutoka katika bendi
ya mjengoni pamoja na nyama choma nzuri na freshi inayotengenezwa na wachoma
nyama waliobobea katika sekta hiyo.
watu wakila bata
huyu ndio mpiga kinanda
Rais wa Bendi ya Mjengoni akiimba kwa hisia
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni