Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya jambazi hilo lililowawa
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi
na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali
ya Monduli kwa ajili ya matibabu.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo alipoongea na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
alisema tukio hilo lilitokea muda saa 07:00 Usiku maeneo ya Makuyuni
barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.
Kamanda Mkumbo
alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na bunduki
ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na marungu
ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya Fusso
lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo likitokea
Moshi kuelekea mkoani Singida.
‘’Mara baada ya kulisimamisha
gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la
Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa Majengo Moshi ambapo
walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung pamoja na fedha taslimu
Tsh 50,000/=’’.
“Wakati wanaendelea na tukio hilo askari
Polisi waliokuwa High Way Patrol walipata taarifa za tukio hilo ambapo
walikwenda kwa haraka na mara baada ya majambazi hao kuwaona walianza
kufyatua risasi hovyo na Polisi kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa
kumjeruhi mmojawao na kuwakamata wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa
na mapanga sita na marungu manne huku wengine akiwemo na yule mwenye
bunduki wakikimbia”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.
Kamanda Mkumbo
alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa haraka, huku
akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila kuvuja jasho
kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni