Waziri
wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo akizungumza na madaktari bingwa wa macho
kutoka Jumuia ya Louis Nielsen ya Denmark ambao wapo Zanzibar kwa ajili
ya kutoa huduma ya miwani kwa wananchi katika Skuli ya Msingi
Kiembesamaki Mjini Zanzibar.
Daktari
Pernille Overgaard kutoka Debmark akimfanyia uchunguzi wa macho Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Skuli ya msingi ya Kiembesamaki.
Wananachi
waliofika Skuli ya msingi ya Kiembesamaki kufanyiwa uchunguzi wa macho
wakiwa kwenye mistari kusubiri zamu zao kuonana na madaktari bingwa wa
macho kutoka Denmark.
Baadhi
ya wananchi waliofanyiwa uchunguzi wa macho na madaktari kutoka Denmark
wakisubiri kupatiwa msaada wa miwani za bure kutoka kwa madaktari hao.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni