RAIS DKT.MAGUFULI ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO UHURU WA HABARI NCHINI


Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Mgufuli  kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu ikiwa ndio kilele chake na kauli mbiu inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.

Ambapo  wageni  zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria  hafla hiyo wakiwepo wadau , wanahabari  ,wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika  inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100  zitawakilisha katika hafla hiyo.

Akizungumza  jjjini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi  ya vyombo vya habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Salome Kitomari amesema katika siku hizo watazungumzia umuhimu wa  uhuru wa habari, utawala bora kwa waandishi wa habari na  wanasheria kama Mahakama kuwa na uhuru  wa kusimamia kesi za jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vilevile na kukumbusha kutekeleza majukumu katika  uandikaji wa habari kuwa sahihi.

Aidha Makamo wa Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji amesema wao wamekuwa na jukumu la kuwaweka pamoja waandishi wa  habari  na kuwapa mafunzo na  kuwapatia  vitendea kazi.

Ametaja baadhi ya vitendea kazi hivyo ni kamera na kompyuta  ili kurahisishia majukumu yao ya kuhabarisha umma ambapo amesisitiza kutokana na uhaba wa vyumba vya habari  mikoani  inakuwa vigumu kupata stori kutoka nje ya Dr es Salaam.Hivyo amesema wamewajengea uwezo  wa mafunzo  ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa rafiki katika utendaji.

"Tumeshuhudia stori ikiwa inatoka lakini katika kufufua maovu yanayotendeka  inaleta  misukosuko, hivyo tunaomba Serikali kuwajibika kufanya kazi yake kwenye upande wa haki na waandishi wa habari kutoa taarifa bila kupendelea mtu na kutoa chukua rushwa,"amesema Mahinja.

Mkurugenzi wa  Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa amesema watashirikiana na wadau wengine kwenye tasnia ya habari kuadhimisha siku hiyo umuhimu na wapo kwa ajili ya kuimarisha vyombo vya habari vinafanya kazi katika mazingira rafiki na kuhakikisha wanahabari kutoa taarifa makini zenye ubora  kwa  jamii.

Kwa upande wa Ofisa habari wa Umoja wa  Wataifa (UN) Stella Vuzo amesema kwa sasa umoja huo unatekeleza maendeleo  endelevu ifika 2030 kila nchi hupaswa kuelezea namna gani imetekeleza hilo lengo na kuhakikisha kuwepo na ushirikiano kwa wanahabari kusaidia kupata taarifa mbali mbali .
Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu na kauli mbiu inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.
Makamu wa Rais wa  Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mahanji akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyokwenda begakwabega na waandishi kwa kuto semina ili kutoa habari zenye faida kwa Taifa.
Mkurugenzi wa  Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa akizungumza na waandishi wa habari wanavyochangia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari kwa kutoa pesa ili vyombo hivyo vijiendeshe.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari kuhusuumoja wa Mataifa unavyodhamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

WAZIRI MPYA WA MAREKANI POMPEO ZIARANI MASHARIKI YA KATI

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo anafanya ziara muhimu kwa nchi washirika wa Marekani katika kanda ya Mashariki ya Kati. Ameanza ziara hiyo kwa kutoa ahadi ya kurejesha mahuasiano mazuri ya kidiplomasia.
Baada ya kuhudhuria mazungumzo ya Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO mjini Brussels, Pompeo anatarajia kuanza ziara ya siku tatu katika nchi za Saudi Arabia, Israel na Jordan ili kuwasilisha mipango ya Rais Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani Pompeo amesisitiza kwamba rais Trump bado hajafanya uamuzi, hata ingawa inategemewa anatarajiwa kuiondoa Marekani katika mkataba huo mwezi ujao, na kuweka tena vikwazo dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo (Reuters/Y. Herman) Waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo
Waziri huyo ambaye zamani alikuwa mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, aliapishwa kama mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Trump mnamo siku ya Alhamis na kisha kuelekea mjini Brussels baada ya masaa mawili amesema atashauriana na wapinzani wa Iran katika kanda ya Mashariki ya Kati kabla ya rais Trump kutoa tangazo rasmi.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson (picture-alliance/AP Photo/A. Harnik) Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson
Waziri huyo mpya wa mambo ya nje amesema binafsi, anataka kuzionesha nchi za nje pamoja na wenzake kwamba diplomasia ya Marekani imerudi upya baada ya uongozi wa wasiwasi wa mtangulizi wake aliyeachishwa kazi bwana Rex Tillerson. Pompeo ameahidi pia kuzungumza na wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje atakaporejea Marekani Jumanne ijayo.
Muda mfupi baada ya kuthibitishwa wakosoaji wamemkosoa bwana Pompeo kwa matamshi yake ya awali dhidi ya Uislamu na pia ndoa za jinsia moja, ambapo wamesema hakuzingatia maadili ya sera za nje za Marekani.
Lakini pia kuna matumaini, katika baadhi ya maafisa wanao andamana naye katika safari hii, kwamba diplomasia ya Marekani sasa imepata mkuu ambaye ataweza kuzungumza kwa niaba ya rais Donald Trump na kuzingatia mipango ya msingi wa wizara ya mambo ya nje.
Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel bin Ahmed Al-Jubeir(Reuters/H. I. Mohammed) Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel bin Ahmed Al-Jubeir
Nchini Saudi Arabia Jumamosi hii, Pompeo atafanya mazungumzo na mwenzake wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir katika jiji la Riyadh, na baadae atakula chakula cha jioni na mwana Mfalme Mohammed bin Salman.
Bin Salman maarufu kama MBS, ndiye mrithi wa mfalme na muanzilishi wa mabadiliko ya kijamii nchini Saudi Arabia na aliyeanzisha mapambano dhidi ya rushwa ili kuwadhibiti wana familia ya kifalme katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Kama Trump na Pompeo, mpinzani mkubwa wa Iran, lakini vita anavyoviunga mkono dhidi ya wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran huko nchini Yemen havina mafanikio na vimechangia maafa makubwa ya kibinadamu nchini humo.
Kushoto: Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Kualia rais wa Marekani Donald Trump (Reuters/JE. Vucci) Kushoto: Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Kualia rais wa Marekani Donald Trump
Rais Trump pia anaitaka Saudi Arabia kuongeza bidii na kuongeza fedha kwa ajili ya kuunga mkono operesheni inayoongozwa na Marekani nchini Syria dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislam ili kuyawezesha majeshi ya Marekani kurudi nyumbani haraka zaidi.
Baada ya ziara ya Saudi Arabia, Pompeo atakwenda Israel kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mshirika wa Marekani, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kisha atazuru Jordan nchi rafiki wa Marekani iliyo na mpaka mrefu baina yake na Syria ambayo inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Huenda Cosby akaozea gerezani

Baada ya miongo kadhaa ya minong´ono, uchunguzi na kesi kufuatiliwa kwa karibu, huenda msanii wa Kimarekani  Bill Cosby akaelekea gerezani akiwa na umri wa miaka 80 kwa makosa ya udhalilishaji wa kingono.
Msanii huyo wa vichekesho alipatikana na hatia  siku ya Alhamisi yya kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mfanyikazi wa Chuo Kikuu cha Temple Andrea Constand katika makazi yake yaliyoko Philadelphia mwezi Januari, 2004.
Wanasheria wanawake  wameutaja uamuzi huo kuwa wa kihistoria. Vuguvugu kwenye mitandao lenye jina #MeToo, limethibitisha kuwa waliokuwa wakimtuhumu Cosby siku zote hawakuwa na makosa: Haiba yake ya uungwana sasa  imevurugwa .
Lili Bernard, aliyesema kuwa Cosby alimdhalilisha kingono kabla ya kumpa nafasi katika kipindi chake maarufu cha "The Cosby Show" mwaka 1992, alijawa na jazba katika mahakama kiasi cha kugonga kichwa chake bila ya kukusudia kwenye meza iliyokuwa mbele yake.
Bill Cosby akiondoka mahakamani Bill Cosby akiondoka mahakamani
"Nimezidiwa na furaha, alisema Bernard nje ya mahakama huku akidondokwa na machozi." Je, nimeamka? Huu ni muujiza."
Zaidi ya wanawake 60 wamelalama kuhusu Cosby
Uamuzi huo, wa kwanza unaomhusisha msanii anayetambulika katika kipindi cha  #MeToo, inahujumu sifa za  msanii mkubwa aliyevuka mipaka ya rangi katika  jukwaa la kuigiza la  Hollywood na kubobea kwenye Televisheni .
Ni moja ya kesi iliotokana na  visa vilivyowakumbuka zaidi ya wanawake 60 waliodai kuwa Cosby aliwapa dawa za kuelevya na kisha kuwadhalilisha kingono kwa kipindi cha miongo mitano, lakini ambao kadhia zao hazikuaminika ama zilipuuzwa kabla ya kuanza kampeni kwenye mitandao ya kijamii yenye anwani #MeToo iliyoangazia dhulma za kingono zilizotekelezwa na wanaume wenye ushawishi mkubwa katika jamii.
Cosby alitumbua macho maelezo ya jaji yakisomwa, lakini baadaye akapaza sauti akimpinga jaji Kevin Steele baada ya mwendesha mashtaka kutaka Cosby apelekwe gerezani mara moja.
Mwendesha mashtaka aliambia mahakama kuwa Cosby ana ndege ya kibinafsi na huenda akiachiliwa akatoroka. Cosby alikanusha kwa hasira kuwa anamiliki ndege na kumtusi mwendesha mashtaka .
Cosby alishtakiwa kwa makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono, kila moja likiwa na kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 gerezani.
Mashtaka hayo huenda yakajumlishwa ama kuunganishwa kwa ajili ya hukumu, lakini ikizingatiwa umri wa Cosby, kifungo chochote kinamaana kuwa huenda akafia gerezani.
Cosby amesema kuwa atakata rufaa
USA Bill Cosby Prozess in Norristown (picture-alliance/newscom/J. Angelillo) Bill Cosby anakabiliwa na makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono
Utekelezaji wa kifungo chake huenda ukafanyika katika kipindi cha miezi mitatu. Kabla ya hayo Cosby lazima afanyiwe uchunguzi kuthibitisha iwapo kuwa ni mtumiaji wa nguvu wa dhulma za kingono. Aidha atajiandikisha kuwa mkosaji wa kingono kwa kuzingatia sheria za Megan.
Jopo la wanaume saba na wanawake watano lilishauriana kwa muda wa masaa 14 kabla ya kutoa uamuzi dhidi ya Cosby.
Constand- 45, mfanyikazi wa Chuo Kikuu cha Temple, alisema Cosby alimlemaza kwa kumpa tembe tatu kisha akakosa fahamu, kisha akamdhalilisha kingono kwa kutumia vidole vyake alipokuwa amelala hana nguvu za kukubali ama kukataa. Cosby anadai kuwa kitendo hicho kiliafikiwa na wote.
Cosby aliupungia mkono umati ambao ulikuwa nje ya mahakama na kuingia kwenye gari lake na kuondoka bila ya kusema chochote. Wakili wake Tom Mesereau alitangaza, "vita havijakamilika" na kusema kuwa atakata rufaa.
Mawakili wa upande Cosby wakiongozwa na Mesereau, aliyeshinda kesi dhidi ya Michael Jackson kuhusu kuwadhalilisha watoto kingono, walishambulia Constand wakati wa kesi hiyo huku wakimuita muongo ambaye alimsingizia Cosby kwa lengo la kutaka kuwa tajiri.

Ellen Johnson Sirleaf kukabidhiwa tuzo ya Mo Ibrahim

Tuzo ya uongozi bora ya Mo Ibrahim kwa viongozi wastaafu barani Afrika kwa mwaka huu inakwenda kwa rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnston Sirleaf. Hafla ya kumtunuku inafanyika mjini Kigali Rwanda.
Mo Ibrahim ambaye amekuwa akitoa tuzo ya uongozi bora kwa viongozi wastaafu barani Afrika amesema bara hilo linakabiliwa na uongozi usiozingatia maslahi ya raia walio wengi huku sekta binafsi ikitelekezwa.
Tuzo ya uongozi bora ya barai Afrika ya Mo Ibrahim ya mwaka huu inatazamiwa badaye jioni ya leo kupewa Rais wa zamani wa Liberia Johnson Sirleaf. Hafla itaongozwa na  Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika, huku akiwepo Rais wa Ivory Coast Alassane Ouatarra ambaye ni mwenyekiti jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika yuko mjini Kigali kuhudhuria khafla hiyo.
Festus Mogae (picture-alliance/ dpa) Rais wa Botswana Festus Mogae, aliwahi kushinda tuzo ya Mo Ibrahim
Mo Ibrahim amesema kwamba kukosekana kwa utashi wa kisiasa na ukosefu wa uongozi kwa maslahi ya raia walio wengi ni jambo ambalo limezuia bara hilo kupiga hatua ya maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
"Hilo ni suala ambalo kamwe huwa halijadili wazi,nani anatoa huduma?nani anatoa elimu,nani anatoa ushirikiano kwenye kila sekta?Ni mwananchi ambaye serikali ambayo wakati haimzingatii kwenye sera zake,hao ni mashujaa ambao daima hatuwazungumzii, na wakati umefika tuwazungumzie", amesema Mo.
Tuzo ya Mo Ibrahim ya dola milioni tano za Marekani hupewa viongozi waliojitahidi kuweka mazingira ya uongozi bora ya utawala wakati wakiwa madarakani.
Hata hivyo tangu ilipoanza kutolewa tuzo hii mwaka 2007  alipotunukiwa  Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano wadadisi wanahisi haijaleta mabadiliko makuwa kwenye sekta za utawala bora barani Afrika, lakini Denittah Ghat ambaye kwenye bunge la Kenya anasema wakati kama huu ni nafasi nyingine ya viongozi kujitathmini ikiwa wanafanya vema katika uongozi.
Kenia Mo Ibrahim verkündet den Gewinner des Preises 2015 (picture-alliance/AP Photo/B. Curtis) Mo Ibrahim mwanzilishi na mwenyekiti wa wakfu wa Mo Ibrahim
"Hii ni nafasi nzuri nay a kipee na ninafurahi kwamba sasa tunakutana hapa kujadili hata nafasi ya mwanamke ktk uongozi barani Afrika tunafahamu kumekuwepo na udhaifu kwa baadhi ya serikali kuwapa nafasi wanawake ambao kimsingi ni wachangiaji wa zuri kwenye maendeleo lakini nadhani kukutana hapa nadhani ni fursa nyingine kulitathmini hili".
Kutolewa kwa tuzo hiyo kumefungua kikao cha siku tatu cha viongozi wa serikali na wale wa kiraia zaidi ya elfu moja kutoka barai Afrika wakijadiliana ushirikiano unaopaswa kuwepo baina ya serikali na sekta binafsi. Rais mstaafu  Sirleaf anapewa tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake katika  kurejesha amani na usalama nchini Liberia na pia hatua yake ya kutojiingiza kwenye siasa za ushawishi kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopita nchini Liberia ambapo mwanasoka wa zamani George Weah  alimshinda aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Joseph Boakai.
Ni tuzo ambayo hutolewa kwa viongozi walioondoka madarakani kwa mujibu wa katiba  au kwa utashi wao. Hata hivyo mwaka  2009,2010,2012,2013.2015 na 2016 jopo la majaji wa wakfu wa Mo Ibrahim lilishindwa kumpata kiongozi  aliyefaa kupokea tuzo hiyo.

Tofali za tope biashara kubwa vijiji vya Kenya

Utengenezaji na uuzaji wa tofali za udongo umejitokeza kuwa mkombozi wa wakazi wa maeneo ya vijijini nchini Kenya, wanaozitumia kwaajili ya kujiingizia kipato, na zinasaidia pia kudhibiti hali ya hewa ndani ya nyumba.
Katika kijiji cha Kivoo mashariki mwa Kenya, Erastus Njiru hutumia njia ya uvuvi wa matope kutengeneza matofali. "Ninaweza kuuza hadi matofali elfu thelathini kwa siku”. Alisema Erastus Njiru mwenye umri wa miaka 34, wakati akisafisha mikono yake iliyokuwa na tope na baadaye kuikausha kwa kutumia taulo.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters Erastus anasema, tofali moja linauzwa kwa shilingi nane za Kenya na kama biashara ikiwa nzuri anaweza kupata shilingi elfu ishirini na nne za Kenya kwa juma moja.
Erastus Njiru ni miongoni mwa wakenya wengi wanaouza na kununua matofali ya tope kwa ajili ya kujengea nyumba ambazo ni za gharama nafuu na zinazoendana na mazingira ikilinganishwa na nyumba zinazojengwa kwa mawe au matofali ya saruji.
Fotowettbewerb KLICK (Ahmad Al-Bazz) Nyumba za tofali za tope zinadhibiti baridi na joto ndani ya nyumba.
Nyumba zaidi zajengwa kwa tofali za udongo
Takribani asilimia 15 ya nyumba mpya kwa sasa zimejengwa na matofali ya tope, ikilinganishwa na asilimia moja ya mwaka 2010 na hiyo ni sawa na kusema kuna ongezeko la asilimia kumi na nne ya nyumba za matofali ya udongo kwa kipindi cha miaka minane tangu mwaka 2010, na hiyo ni kwa mujibu wa afisa mkuu katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya mijini, Aidah Munano.
Mahitaji ya matofali ya tope kwa Kenya yapo katika maeneo ya vijijini zaidi kwa sababu nyumba zilizojengwa kwa matofali hayo zinaweza kutoa baridi wakati wa joto na kutoa joto wakati wa usiku, na gharama yake ni nusu ya ile ya matofali yaliyotengenezwa kwa saruji au mawe. Hiyo ni kwa mujibu wa Gitonga Murungi, muhifadhi kutoka Kenya.
Inaelezwa kuwa watu wa maeneo hasa ya vijijini nchini Kenya wanaogopa kujenga nyumba zao kwa kutumia mawe kwa gharama kubwa ikilinganishwa na matofali ya tope.
Indien Arbeiter in einer Ziegelfabrik 12.01.2015 (Reuters/N. Chitrakar) Utengenezaji wa tofali za tope umekuwa chanzo cha mapato kwa Wakenya wengi waishio katika maeneo ya vijini.

Chanzo cha ada ya watoto
Mmoja kati ya wakulima wa zamani nchini Kenya anasema kuwa yeye hakupata nafasi ya kumaliza masomo yake ya shule ya sekondari kwa sababu ya kukosekana kwa pesa za kulipa ada ya shule, lakini kwa sasa yeye anaweza kumudu gharama za kuwasomesha watoto wake mpaka chuo kikuu kwa biashara hiyo ya kuuza matofali ya tope.
Ayubu Shaka, mkurugenzi msaidizi wa idara ya hali ya hewa Kenya amesema kuwa upepo mkali sana katika nchi ya Kenya ni kitisho kwa raia kwa sababu mazao na mifugo wanapotea kwa kukosekana kwa maji.
Kuongezeka kwa joto kumemsababisha Milka Njeri mkulima wa mtama nchini humo kuzingatia utengenezaji wa matofali kama chanzo kingine cha mapato ya ziada. Anasema hapati pesa nyingi lakini si haba kwani anaweza kupata shilingi 2000 za Kenya kwa juma moja.
Watengenezaji wa matofali ya tope wanashauriwa kuhakikisha kuwa kazi yao haiharibu mazingira alisema Violet Matiru mhifadhi katik ashirika la misaada linalojihusisha na kutoa eleimu kuhusu masuala ya mazingira.

PROFESA KABUDI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA



Na Munir Shemweta, Morogoro

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha watumishi katika mipango ya uendeshaji Taasisi kwa kuwa suala hilo lipo kisheria.

Aidha, alisema kwa miaka yote Serikali imekuwa ikisisitiza Taasisi kujenga na kutekeleza utaratibu wa kushirikisha watumishi na hali hiyo inatokana na ukweli kuwa palipo na watumishi wengi pana mawazo mengi.Profesa Kabudi alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa kumi na tatu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.

‘’Ushirikishwaji watumishi kwenye mipango ya uendeshaji ofisi unasaidia kupata mawazo mengi na mapya yanayoweza kurahisisha uendeshaji wa ofisi na kutoa fursa ya kusikiliza kero na changamoto kwenye uendeshaji wa Taasisi na kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi’’ alisema profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa, kwa kushirikiana na watumishi ni dhahiri wanapata morari wa kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa mipango ya taasisi ambayo wao wenyewe walishiriki kuiandaa.Waziri huyo wa Katiba na Sheria alisema, ushirikishwaji unafanywa kupitia baraza la wafanyakazi kwa kuwa baraza ni chombo kinachowashirikisha wafanyakazi katika kupanga , kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali inayohusu shughuli za kazi za Taasisi kama zilivyoainishwa katika sheria za nchi.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, Mabaraza hutoa fursa kwa wafanyakazi kushiriki katika maamuzi mbalimbali na kuboresha uhusiano baina ya wafanyakazi na uongozi pamoja na mazingira ya utendaji hasa mahala pa kazi hivyo baraza ni chombo cha kuimarisha na kuboresha demokrasia mahala pa kazi.

Amewataka wajumbe wa baraza wa Tume ya Kurekebisha Sheria kuzingatia suala la nidhamu kazini, misingi ya kazi na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu. Aidha, alitaka uzembe kazini upigwe vita na suala la kufanya kazi kwa mazoea kukomeshwe na kubainisha kuwa,vipaumbele viwekwe katika kulinda rasilimali za Tume na kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na mali zake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria ambaye ni Katibu Mtendaji Tume Casmir Kyuki alisema katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018 Tume yake imeweza kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika bajeti.

Ameyataja majukumu hayo kuwa ni kufanya mapitio ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Haki Jinai, Sheria ya Ushahidi, Uchambuzi wa Kesi za Mahakama ya Rufaa, Mfumo wa Sheria Unaosimamia Huduma ya Ustawi wa Jamii, Mfumo wa Sheria za Ufilisi pamoja na kutoa elimu ya sheria kwa umma.

Ameishukuru serikali kwa mabadiliko makubwa iliyoyafanya katika sekta ya sheria kupitia tangazo la serikali namba 48,49 na 50 ambapo yameleta muundo mpya kwa kuanzishwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai na ile ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume Casmir Kyuki na kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Casmir Kyuki (Kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Khalist Luanda mara baada ya kufunguka mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume (Idara ya Mapitio) Angelah Bahati (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Sehemu ya Wajumbe Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.


MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi. Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi. 

Aidha, akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao. 


Mfuko umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018. 
Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw. Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza