Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikata utepe kuashiria Uzinduzi Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na
Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine
pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe
(kulia),Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodrigues
na kushoto ni Muendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga na
Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu) Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad
Masauni Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa
Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, katikati ni Muendesha Mashitaka
Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais -
Ikulu)Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha
Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais - Ikulu)
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Makamu wa Rais Samia Suluhu azindua muongozo kwa watumishi katika kesi za wanyamapori.
MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha mashitaka, polisi na
wapelelezi wa kesi za wanyamapori na misitu kubadilika katika kazi zao
ili kulinda rasilimali hizo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Aidha,
ameitaka mahakama kutoa muongozo kwa watumishi wake kuhusu namna ya
kuendesha kesi zinazohusiana na nyara za serikali kwa lengo la kuwa na
uwiano sawa katika utoaji amri.
Samia
amesema hayo leo mjini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwongozo kwa
wapelelezi, waendesha mashitaka na Polisi wa kesi za wanyamapori na
misitu ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).
Amesema
wote hao wanatakiwa kufanya kazi zao ipasavyo kuhakikisha usalama wa
wanyamapori na misitu kwani kwa kupoteza maloiasili hizo kunafanya
uchumi wa nchi kushuka na kwamba wasifanye kazi hiyo kwa kuweka
mazingira ya rushwa.
Amesema,
kazi za kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapori zimekuwa na
ushawishi mkubwa wa rushwa kutoka kwa wahusika na kuwataka kufikiria
maslahi mapana ya nchi na sio wao binafsi.
"Jamani,
msiogope kufa, kifo kipo na kila mmoja wetu atakufa hata mnyama ikiwemo
huyo FaruJohn, muhumu ni namna ya kujua aina ya kifo utakachokufa,
lakini Jambo la kusikitisha mmekuwa mkiponzwa na fedha, wahenga walisema
'fedha ni sabuni ya roho lakini pia walisema fedha ni fedheha," amesema
Samia.
ameongeza
kuwa, Rais Magufuli ana lengo kubwa la kulinda maliasili za nchi hii na
kwamba kutaka kwake kuwepo kuwepo kwa miongozo hiyo katika mahakama
kutasaidia mahakimu na majaji kutoa adhabu na dhamana zinazowiana.
Ameongeza,
mara kadhaa kumejitokeza majaji na mahakimu kutoa adhabu
zinazotofautiana au masharti yanayo tofautiana katika kesi zenye
mazingira sawa.
Aidha
amemtaka DPP kufanya namna ya kuwapeka watumishi hao kwenye mbuga za
wanyama, vyanzo vya maji na maeneo ya mbali mbali yenye misitu ili
kujionea ni kwa namna gani rasilimali za nchi zinavyopotea kwa wanyama
kuuawa kwa kukosa maji.
Amesema,
mwongozo huo uliotolewa utasaidia kuboresha upelelezi na uendeshaji wa
mashitaka na kwamba mapambano dhidi ya ujangili na uhalifu yatakoma na
matokeo chanya yatakuwa yakipatikana katika kesi mbali mbali na serikali
kuweza kupata mapato yake katika sekta ya utalii.
Akitoa
takwimu za sekta ya wanyamapori, Samia amesema, Taasisi ya Utafiti wa
Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ya mwaka 2009, ilionesha kuwa Tanzania
ilikuwa na tembo 109,051 na sensa ya mwaka 2014 ilionesha idadi ya tembo
imepungua na kufikia tembo 43,330 ambao sawa na asilimia 60.3 ya tembo
wote.
Alisema
sababu kuu ya kupungua kwa tembo hao ni ujangili na kwamba takwimu
rasmi za Sekretarieti ya Maktaba wa Kimataifa unaoratibu biashara ya
wanyama waliohatarini kutoweka (CITES), ilionesha asilimia 70 ya meno ya
tembo yaliyokamatwa duniani kote kati ya mwaka 2008 na 2013, yalitokea
Afrika Mashariki nchi za Tanzania na Kenya ambapo kiasi kikubwa
kilitokea Tanzania.
Kwa
mujibu wa sensa ya Taasisi ya International Union for the Conservation
of Nature (IUCN) ya mwaka 2013, Tanzania ilishuka hadi namba tatu kwa
idadi ya tembo kwa asilimia 13 ya tembo wote waliopo barani Afrika ikiwa
nyuma ya Botswana (asilimia 33) na Zimbabwe (asilimia 16).
Naye
DPP Biswalo Mganga amesema katika kipindi cha mwaka 2014 na 2017,
washitakiwa 100 walihukumiwa kulipa faini ya bilioni 1.1 na vifungo
virefu ambazo tayari imeshalipwa serikalini.Aidha, watuhumiwa 80
walihukumiwa kifungo cha miaka 20 na 30 gerezani na faini ya bilioni
164.7 ambayo bado haijalipwa.
Alisema
suala la dhamana kwa makosa makubwa yanayohusu wanyamapori
waliohatarini kutoweka ikiwemo tembo na faru, watuhumiwa wengi wamekuwa
wakitoroka na kusababisha kesi kutoendelea dhidi yao.
Ameongeza
mwaka kati ya 2010 na 2015 mashauri 13 yanayohusiana na nyara za
serikali zenye thamani ya milioni 800 yalifikishwa katika Mahakama za
Mkoa wa Dar es Salaam lakini watuhumiwa wake walitoweka baada ya kupewa
dhamana.
Hata
hivyo, alisema asilimia 69 ya watuhumiwa hao ni raia wa kigeni na
asilimia 31 ni Watanzania; wakati mahakama inapotoa dhamana, moja ya
masharti yake ni kunyang'anywa hati zao za kusafiria.Alifafanua kuwa
kati ya kesi hizo 13 watuhumiwa waliua jumla ya tembo 300, chui nane,
Kobe 210, twiga,kiboko, pundamilia na ndege wa aina mbalimbali wenye
thamani ya milioni 800.
Amesema,
takwimu zinaonesha kuwa asilimia 70 ya washitakiwa huruka dhamana na
kukimbia kesi pindi wanapopewa dhamana kwa hiyo, anajitahidi kuchukua
hatua madhubuti kwenye suala la dhamana hasa kwenye kesi zinazohusu meno
ya tembo na faru wanaokaribia kutoweka nchin.