Mwenyekiti
wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah katikati akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Tanga leo kuhusu bei elekezi ya korosho msimu
wa 2017/2018 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni
Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Maokola Majogo
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akizungumza katika mkutano huo kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)Hassani Jarufu
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia
Waandishi
wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku
Yusuph wa Gazet la Tanzania Daima,Amina Kingazi wa Gazeti la The
Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub wa Mwananchi
Sehemu
ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kulia ni
Sussan Uhinga wa gazeti la Mtanzania Tanga,Pamela wa Tanga One Blog
wakifuatilia
Mwandishi wa gazeti la Habari Leo mkoani Tanga Anna Makange akiuliza swali kwenye mkutano huo
Mwandishi wa Clouds TV Mkoani Tanga Gift Kika akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania
BODI
ya Korosho Tanzania imetangaza bei elekezi kwa msimu 2017/2018 kwa kilo
moja ya Korosho ghafi daraja la kwanza (Standard Grade) kitakuwa ni
sh.1,450 huku kilo moja ya daraja la pili itakuwa ikiuzwa kiasi cha
sh.1,160.
Hayo
yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati
akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa
soko la Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.
"Niseme
tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka
waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada
ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho
ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.
Alisema
kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni
1,208.39 na asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .
Aidha
alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018
ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama
cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya
sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni
143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni
tsh.1,593.50.
Aliongeza
kuwa katika msimu wa ununuzi wa korosho 2017/2018 utafunguliwa rasmi
Octoba Mosi mwaka huu huku akiwahimiza wadau wote wanaohusika na uuzaji
na ununuzi wa zao la korosho kukamilisha maandalizi ya msimu kabla ya
ununuzi kuanza.
"Wadau
hao ni pamoja na Sekretarieti za mikoa,halmashauri za
wilaya,Wakulima,Vyama vya Ushirika vya Msingi,Vyama Vikuu vya
Ushirika,Wakala wa Vipimo,Bodi ya Leseni za Maghala,Waendesha
Maghala,Wasafirishaji,Wanunuzi,Mamlaka ya Bandari,Mabenki na wengine
ambao wanahusika kwa namna moja au nyengine"Alisema.
Akizungumzia
suala la utoaji wa leseni za ununuzi wa korosho, Mwenyekiti huyo
alisema bodi hiyo inatumia fursa hiyo kuwahamasisha wanunuzi wa zao hilo
wa ndani na nje kuomba leseni ya ununuzi kwa ajili ya msimu wa
2017/2018.
"Leseni
hii itatolewa bila malipo yeyote,Fomu namba 2 ya maombi ya leseni za
ununuzi wa korosho ghafi inapatikana kwenye tovuti ya bodi ya korosho
Tanzania (www.cashew.go.tz) na kwenye ofisi zake zilizopo Mtwara(Makao
Makuu) na kwenye matawi yake ya Dar es Salaam,Tanga na Tunduru "Alisema
Hata
hiyo alisisitiza umuhimu wa wauzaji,wanunuzi na wadau wa korosho kufuata
mfumo wa stakabadhi ghalani wa kuuza na kununua korosho huku akitoa
wito kwa yeyote atakayekiuka sheria,kanuni na mwongozo namba 1 wa mwaka
2017/2018 wa mauzo ya korosho,atachukuliwa hatua kali ikiw ni pamoja na
kutaifishwa korosho.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijami ya Tanga Raha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni