Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwa katika
mazungumzo na Mkuu wa BBC, Idhaa ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania,
Bw. John Solombi leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. Timu ya
BBC imeanza ziara kuwatembelea wadau wake wakubwa katika masuala ya
kupashana habari na wameanza kwa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje na
baadaye walielekea kwa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini. Katika
mazungumzo hayo, wawili hao walikubaliana kufanya kazi kwa karibu kwa
maslahi ya kuuelimisha na kuuhabarisha umma.
Bw. Solombi akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
Mazungumzo
yanaendelea. Katika picha anaonekana Bw. Aboubkar Famau, Mtangazaji wa
BBC na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Vipindi, akichangia jambo katika
mazungumzo hayo. Kulia kwake ni Bw. Ally Kondo, Afisa Mawasiliano wa
Wizara ya Mambo ya Nje na aliyekaa peke yake ni Bi. Halima Nyanza,
Mtangazaji wa BBC.
Picha ya pamoja
Timu
ya BBC baada ya kukutana na Kitengo cha Mawasiliano ilipata fursa ya
kusalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb). Pichani anaoenekana Mhe. Naibu
Waziri akiwapa neno la shukrani Team ya BBC kwa uamuzi wao wa kuichagua
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa mdau wa
kwanza kutembelewa.Mhe. Naibu Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Team ya BBC na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni