Kiwavijeshi aina ya Fall Armyworm (FAW).
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Wizara
ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imeanza jitihada za kuwakabili Viwavijeshi
wapya aina ya Fall Armyworm (FAW) wanaojulikana kitaalamu kama
Spodoptera Frugiperda ambao wametajwa kuwa na uwezo mkubwa kuharibu
mazao mbalimbali hususan mahindi ambayo ndio zao kuu la chakula nchini.
Imeelezwa
kuwa Viwavijeshi hao wanapofika kwenye mazao hutoa kemikali ambayo
huweza kudanganya mmea kuwa unashambuliwa na magonjwa kama ukungu au
fangasi hivyo mmea unapohisi unashambuliwa na hayo magonjwa, hupunguza
kinga dhidi ya wadudu hao hatari na kuwa rahisi kushambuliwa.
Hayo
yamebainishwa leo Septemba 14, 2017 na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus
Malema wakati akifungua warsha ya siku moja mbele ya Wadau wa Kilimo
ambao ni Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani USAD, ONE HACKER FUND,
Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA .
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi, Bwana Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku
moja kujadili namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.
Mkutano
ulikuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja kwa ajili ya kumkabili
mdudu huyo aina ya Fall Armyworm (FAW) ambaye anashambulia mazao
mbalimbali nchini hususani zao la mahindi.
Alisema
Athari ya viwavi jeshi haishii kuharibu majani ya mimea pekee, wadudu
hao wanapokula majani na kutengeneza sumu aina ya ‘firenide’ inayodhuru
mifugo inapokula majani yaliyoathiriwa.
Bwana
Malema amesema tayari Serikali imechukua juhudi za awali kukabiliana na
mdudu huyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utambuzi
wa mdudu huyo kwa kuwataka Wananchi kung’oa mazao na kuyachoma pindi
wanapobaini uwepo wa mdudu huyo.
Pia
tayari dawa tatu zimepitishwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
kupitia Taasisi ya uchunguzi wa Viatilifu (TPRI) zinazoangamiza wadudu
hao ambazo ni Duduba 450, Mupacrone 500 EC na Match Save kutoka Kampuni
ya Syngenta hivyo Wananchi wametakiwa kuzitumia haraka pindi wanapoona
dalili za kuwepo wa wadudu hao shambani.
Wadau wa
kilimo kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani Wizara ya Kilimo
Mifugo na Uvuvi, USAD, ONE HACKER FUND, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu
Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana
Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kujadili
namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.
Bwana
Malema amesema kuwa katika kipindi cha miaka mingi Tanzania imekuwa
ikikumbwa na viwavijeshi aina ya African Armywarms ambapo mara zote
imekuwa ikiwadhibiti wadudu hao wanapojitokeza kwa kuwapa kiuatilifu
kinachosababaisha matumbo ya wadudu hao kujaa na hatimaye kuwasababishia
vifo.
Ameongeza
kuwa kwa mara ya kwanza Wizara ilipata taarifa ya uvamizi katika shamba
la Mwekezaji mkubwa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017 na
walipofuatilia na kupeleka sampuli maabara mdudu huyo alibainika kwa
jina la Spodoptera frugiperda au Fall arymworm ambaye ni hatari na
amekuwa akiripotiwa katika maeneo mbalimbali duniani.
Kutokana
na unyeti wa suala hilo Wizara ya Kilimo imewasiliana na Shirika la
Chakula Duniani (FAO), kwa ajili ya kuunganisha juhudi za pamoja ili
kumdhibiti mdudu huyo kabla hajasambaa kwenye maeneo mengi nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Mimea, Idara ya Maendeleo ya Mazao katika
Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bibi Beatrice Palangyo akiwasilisha
mada ya utambuzi wa Viwavijeshi wapya aina ya Fall Armyworm (FAW)
wanaojulikana kitaalamu kama Spodoptera Frugiperda wakati wa warsha ya
kujenga uelewa juu ya wadudu hao.
Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika taarifa yake
imesema viwavijeshi hao aina ya Fall armyworm wameonekama pia katika
nchi za Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Namibia Afrika ya Kusini na Zambia
huku chanzo chake ikiwa ni nchini Marekani.
Kwa
mujibu wa Redio ya Umoja wa Mataifa, FAO bado haijatangaza kiwango
kamili cha uharibifu katika nchi hizo, huku ikiongeza kuwa Shirika hilo
na Wadau wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
wamejadili udhibiti wa viwavijeshi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Mimea, Idara ya Maendeleo ya Mazao
katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bibi Beatrice Palangyo
akiwasilisha mada ya utambuzi wa wadudu hao katika warsha hiyo amesema
kuwa katika Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wadudu hawa walianza
kuingia nchini Nigeria na kwa sasa wameenea katika nchi mbalimbali
ikiwemo Tanzania, Afrika kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na
Malawi.
Alisema
wadudu hao wanashambulia mazao ya jamii ya nafaka kama mahindi (Corn)
wanauwezo wa kushambulia hata magugu pale wanapokosa mazao kama mahindi
kwani hawali mazao mengine kama mboga na matunda, wanakula zaidi mahindi
na magugu yanayofanana na mahindi.
Zaidi
ya Mikoa 15 nchini ikiwemo Zanzibar imeripoti kuwepo kwa kadhia ya mdudu
huyo hivyo asilimia 15 ya mazao jamii ya nafaka kama mahindi
yameathiriwa, jambo ambalo kama lisingepatiwa ufumbuzi wa haraka,
lingesababisha upotevu mkubwa wa mazao mashambani na kutishia
upatikanaji wa chakula nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni